Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 05/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 05/2020

SIKU 24 YA 31

Nawaandikia haya ili ... (m.1). Angalia! Mwandishi wetu anamwandikia Mkristo wa kweli anayeenenda nuruni, yaani mtu anayeishi na Mungu kwa maisha yake yote. Ingawa tumeshasafishwa tayari na damu yake Yesu (1:7b,Damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote), twaanguka dhambini, kwa kuwa bado tupo katika ulimwengu huu. Tunaye mwenye haki, yaani, Kristo, ambaye ni Mwombezi kwa Baba. Bado anaendelea kutusafisha na damu yake, bado anatusamehe dhambi zetu tukianguka. Ili ... msitende dhambi (m.1): Nuru na giza havipatani! Siyo kweli shetani akisema hakuna shida: "Siyo hatari kutenda dhambi kwani tunao ukombozi!" Tusimsikilize.

siku 23siku 25

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 05/2020

Soma Biblia Kila Siku 05/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Ayubu, Zaburi na 1 Yohana. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz