Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 06/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

SIKU 25 YA 30

Wale ambao hawakucheza ni Yohana na wanafunzi wake. Yohana na wanafunzi wake walitumia sana kufunga (taz. m.18:Yohana alikuja, hali wala hanywi). Kwa hiyo walidai ana pepo. Wale ambao hawakulia ni Yesu na wanafunzi wake, maana kukaribia kwa ufalme wa Mungu ni neema kubwa, ni furaha ya ajabu (taz. m.19:Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywarafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi!) Katika Mit 8:12-36 kuna unabii juu ya Yesu Kristo. Katika unabii huu Kristo anajitambulisha kwa kujiita "Hekima" kama anavyofanya hapa katika m.19b: Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa kazi zake. Kazi yake Yesu inamshuhudia yeye ni nani. Hata hivyo wengi hawakutubu, Yesu anasema katika m.20-24:Ndipo akaanza kuikemea miji ile ambamo ndani yake ilifanyika miujiza yake iliyo mingi, kwa sababu haikutubu...

siku 24siku 26

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz