Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Naweza Kweli Kushinda Dhambi na Majaribu?Mfano

Can I Really Overcome Sin and Temptation?

SIKU 1 YA 5

Je, Kweli Ninaweza Kushinda Dhambi na Majaribu?

Katika 1 Samweli 13:14, nabii Samweli anamwambia Sauli, mfalme wa Israeli, kwamba atachukuliwa mahali pake kwa sababu “Bwana amejitafutia mtu aupendezaye moyo wake, naye Bwana amemuru yeye kuwa mkuu juu ya watu wake."

Hata hivyo, miongo kadhaa baadaye, “mwanaume anayeupendeza moyo wake” ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamke aliyeolewa, na kusababisha mimba, na kufanikisha njama ya kumuua mume wake ili amchukue mwanamke huyo kama mke wake.

Katika tukio hili moja, Mfalme Daudi alivunja tisa kati ya Amri Kumi:

10: Alimtamani mke wa jirani yake.

9: Alidanganya kuhusu dhambi yake.

8: Aliiba kwa ajili yake mwenyewe.

7: Alifanya uzinzi.

6: Alimuua mumewe.

5: Aliwavunjia heshima wazazi wake.

2 Alitengeneza sanamu ya Bathsheba.

1 na 3: Alimwaibisha Mungu na jina lake.

Angalau Daudi hakuvunja Sabato—kama tunavyojua.

Kwa nini mtu aliyeupendeza moyo wa Mungu alifanya hivi?

Kwa nini tunatenda dhambi? Je, tunashindaje majaribu? Tunafanya nini tusipofanya hivyo?

Haya ndiyo tutakayojadili katika siku nne zijazo.

Tarajia Kujaribiwa

Yesu aliposhinda mashambulizi ya Shetani, adui “akamwacha mpaka wakati ufaao” (Luka 4:13). Ikiwa Bwana wetu alikumbana na majaribu, vivyo hivyo na sisi.

Ibilisi ni halisi sana, na anakuchukia. Wewe ni adui yake. Yesu alituonya kwamba shetani ni “mwuaji tangu mwanzo,” na “mwongo na baba wa uongo” (Yohana 8:44). Yeye ni “simba angurumaye akitafuta mtu ammeze” (1 Petro 5:8). Anamjaribu na kumdanganya kila mmoja wetu.

Hii ndiyo sababu: “Tamaa ikiisha kuchukua mimba, huzaa dhambi; na dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti” ( Yakobo 1:15)

Angalia: dhambi daima hukupeleka mbali zaidi ya ulivyotaka kwenda, hukuweka muda mrefu zaidi ya ulivyotaka kukaa, na inakugharimu zaidi ya ulivyotaka kulipa.

Daima.

Muulize tu Mfalme Daudi. Soma 2 Samweli 12 kwa matokeo mabaya.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Can I Really Overcome Sin and Temptation?

Umewahi kujiuliza, “Mbona bado napambana na dhambi hiyo?” Hata mtume Paulo alisema hivyo katika Warumi 7:15: “ Sifanyi ninachotaka, lakini nafanya kile ninachochukia.” Je, tunazuiaje dhambi kusimamisha maisha yetu ya kiroho? Je, hata inawezekana? Hebu tujadili dhambi, majaribu, Shetani, na, kwa shukrani, upendo wa Mungu.

More

Tungependa kumshukuru Denison Forum kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.denisonforum.org

Mipango inayo husiana