Soma Biblia Kila Siku 11/2020Mfano
![Soma Biblia Kila Siku 11/2020](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans-staging%2F22531%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Masihi, yaani Kristo, alisubiriwa na Waisraeli tangu muda mrefu. Alitazamiwa kuwa ataikomboa Israeli dhidi ya mateso yote. Maandiko yaliwaambia atakujaje na ataonekanaje. Ujio wake utaleta mapinduzi ya watu kuponywa magonjwa, kusamehewa dhambi na kubarikiwa kwa baraka mbalimbali. Lakini alipokuja hawakumtambua. Kwao Yesu alionekana ni mwana wa mtu tu wala si Mwana wa Mungu. Basi, ni vema kuendelea kukaa katika Neno la Mungu, ili ajapo, atukute tupo tayari kumpokea.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![Soma Biblia Kila Siku 11/2020](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans-staging%2F22531%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Soma Biblia Kila Siku 11/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz