Soma Biblia Kila Siku 12/2020Mfano
Msifuni Mungu(m.1). Zaburi ya mwisho inaonyesha kilele na jambo kuu la kitabu chote cha Zaburi. Msifuni kwa matendo yake makuu (m.2). Imetupasa kumsifu Mungu aliyeumba mbingu na dunia, anayetutunza na kutupenda, aliyefanya mambo mengi makuu kwa ajili yetu, na aliyetuokoa kwa Mpatanishi wetu. Watu wote na viumbe vingine vyote hushirikiana katika kumsifu Bwana Mungu kwa ukuu wa nafsi yake na kwa matendo yake! Kwa kila njia iwezekanayo watu wote wa kila mahali wamsifu Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wathesalonike, Mathayo na Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz