Soma Biblia Kila Siku Februari 2021Mfano
Hasira na ghadhabu ya Mungu yatisha sana. Tuungame na mtunga zaburi hii kumwomba Mungu tusiangukie katika hasira yake. Jambo la muhimu sana pia, ni kuyajua na kuyaepuka yote yaletayo hasira ya Mungu. Je, unayajua? Soma Neno la Mungu (k.mf. Efe 5:1-7), utayajua! Je, umeyashika uliyoyasoma? Kumbuka pia, Mungu anapokurudi na kukukemea anakupenda (ling. Ebr 12:5-6,Mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, Wala usizimie moyo ukikemewa naye;Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi). Yakupasayo Mungu akikukemea na kukurudi ni kutubu dhambi, kunyenyekea, na kutii. Hapo ndipo Mungu atakuponya na kukukweza kwa wakati wake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Februari 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz