Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoMfano

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

SIKU 24 YA 40

Tunapoendelea kusoma, tunaona vuguvugu la Yesu likiendelea kuongezeka kwa kasi, Wayahudi kutoka mataifa mengine wanapoanza kumfuata Yesu. Wanapopokea uwezo wa Roho Mtakatifu, maisha yao yanabadilika, na jamii inaanza kuishi kwa njia mpya kabisa, ikiwa imejawa furaha na ukarimu. Wanakula vyakula vya kila siku pamoja, wanaomba pamoja mara kwa mara, na hata wanauza vitu vyao ili kuwasaidia maskini walio miongoni mwao. Wanajifunza maana ya kuishi chini ya agano jipya, ambapo uwepo wa Mungu unaishi ndani ya watu badala ya hekalu.

Huenda unajua kuhusu simulizi ya ajabu katika kitabu cha Walawi kuhusu makuhani wawili waliomkosea Mungu heshima katika hekalu na kisha wakafa ghafla. Katika somo lililoteuliwa la leo, Luka anasimulia simulizi inayofanana na ile ya Walawi kuhusu watu wawili waliotia fedheha hekalu jipya la Roho Mtakatifu na kufa. Wanafunzi wanatiwa hofu. Wanaelewa uzito wa hili agano jipya, hivyo wanapokea onyo hilo, na uovu katika hekalu jipya unaondolewa. Lakini uovu katika jengo la hekalu la zamani unaendelea kadiri viongozi wa dini wa hekalu wanavyoendelea kupambana dhidi ya wafuasi wa Yesu na ujumbe wake. Kuhani mkuu na maafisa wake anatishiwa sana na mitume hadi anawafunga gerezani tena, lakini malaika anawaondoa kwenye gereza na kuwaambia waende hekaluni ili kuendelea kushiriki ujumbe wa Ufalme wa Yesu. Viongozi wa dini wanasisitiza kuwa mitume waache kuhubiri kuhusu Yesu lakini mitume wanaendelea. Kufikia hapa, viongozi wa dini wako tayari kuwaua mitume, lakini kiongozi anayeitwa Gamalieli anawakomesha kwa kusema kuwa ikiwa ujumbe wao unatoka kwa Mungu, hakuna chochote kitakachoweza kuuzuia.

siku 23siku 25

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.

More

Tungependa kuwashukuru BibleProject na YouVersion kwa kutupa somo hili. Kwa taarifa za ziada, tafadhalo tembelea: www.bibleproject.com na www.youversion.com