Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

SIKU 27 YA 31

Lengo la mfano huu wa mamba na nguvu zake laonekana katika m.11 Mungu anapotukumbusha: Kila kilicho chini ya mbingu nzima ni changu. Nguvu za mamba zashuhudia uwezo mkuu wa Mungu aliyemwumba. Mungu amejitosheleza kwa vitu vyote. Sisi twavuna kutoka kwake sehemu ndogo ya vipawa vyake vifanyike msaada kwetu, watoto wetu na ndugu zetu. Zab 125:1 yatia muhuri ukweli huu ikisema: Wamtumainio Bwana ni kama mlima wa Sayuni, ambao hautatikisika, wakaa milele. Kila aishiye kwa tumaini la kuwezeshwa na Bwana hataishiwa matumaini wala kujuta. Mtegemee Mungu, mweza wa vyote na mpaji wa vyote.

siku 26siku 28

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

Mipango inayo husiana