Soma Biblia Kila Siku Mei 2021Mfano
Yesu akajitenga, yeye na wanafunzi wake (m.7). Habari za Yesu zilipozidi kuenea, umati wa watu ulimfuata. Kwa hiyo ikabidi wakati fulani Yesu na wanafunzi wake wapate kukaa peke yao ili wapumzike na ili Yesu apate kuwafundisha. Umati ulipozidi, Yesu akawachagua mitume 12 kati ya wanafunzi wake ili wamsaidie katika kazi yake. Neno muhimu la kuzingatia ni kwamba wajibu wa kwanza wa mtumishi wa Bwana si kuhubiri wala kutoa pepo, bali ni kuwa pamoja naye (m.14, Akaweka watu kumi na wawili, wapate kuwa pamoja naye, ...). Huu ndio msingi! (Ukiwa na nafasi, tafuta kusoma Yn 15:4-8 ambapo Yesu anakaza jambo hilo hilo akitumia mfano wa mzabibu na matawi yake).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Mei 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz