Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022Mfano
“Ulimwengu wa roho” (m.3) ni ule wa mbinguni ambapo Kristo anatawala baada ya kufufuka. Hapo wapo pia waumini ambao kwa neema yake Mungu wamefufuka na Kristo kutoka kwenye dhambi ambapo Kristo amewafufua pamoja naye, akawaketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho (Waefeso 2:6). Kutoka hapo wanabarikiwa kwa baraka zote. Uchaguzi (m.4,Kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu) ni uamuzi wa Mungu kufuatana na mapenzi yake matakatifu. Ametuchaguakatika Kristo! Hivyo uchaguzi wake ni imara, na utatekelezwa kwa uhakika, kwa kuwa unamtegemea Yesu wala si mimi na wewe. Rudia m.4 ukitafakari zaidi lengo la uchaguzi wa Mungu:Kama vile alivyotuchangua katika [Kristo] kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kushukuru Soma Bible kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/