Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 2 - Matendo ya MitumeMfano

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

SIKU 1 YA 20

Luka ni mwandishi wa simulizi ya kwanza kabisa kuhusu maisha ya Yesu, kifo, kufufuka, na kupaa kwake kurudi mbinguni, tunaita maelezo haya, Injili ya Luka. Je, ulijua kuwa Luka pia ana toleo la pili? Tunalijua kama kitabu cha Matendo ya Mitume. Toleo hili linahusu mambo ambayo Yesu aliyefufuka anaendelea kuyafanya na kufundisha watu wake kupitia Roho wake Mtakatifu baada ya yeye kupaa kwenda mbinguni.

Kitabu cha Matendo ya Mitume kinaanza na mkutano baina ya wanafunzi na Yesu aliyefufuka. Kwa wiki kadhaa, Yesu anaendelea kuwafundisha kuhusu Ufalme wake unaoenda kinyume na matarijio na uumbaji mpya aliozindua kupitia kifo chake na kufufuka kwake. Wanafunzi wanataka kwenda na kushiriki mafundisho yake, lakini Yesu anawaambia wasubiri hadi wapokee aina mpya ya uwezo, ili waweze kuwa na kila wanachohitaji waweze kuwa mashahidi waaminifu wa Ufalme wa Yesu. Anasema kwamba misheni yao itaanzia Yerusalemu, kisha kwenda hadi Yuda na Samaria, na kisha kutoka hapo hadi kwa mataifa yote.

Dhamira kuu na usanifu wa kitabu cha Matendo ya Mitume unajitokeza katika sura hii ya ufunguzi. Hii ni simulizi inayoonyesha Yesu akiwaongoza watu wake kupitia Roho wake ili kuyaalika mataifa yote kuishi ndani ya mapenzi na uhuru wa Ufalme wake. Sura saba za kwanza zinaonyesha jinsi mwaliko utaanza kuenea ndani ya Yerusalemu. Sura nne zinazofuata zinaelezea jinsi ujumbe unavyoeenea kwa wale wasio Wayahudi katika maeneo yaliyo karibu na Yuda na Samaria. Na kuanzia sura ya 13 kuendelea, Luka anatuambia jinsi habari njema za Ufalme wa Yesu zinaanza kufikia mataifa yote ya ulimwengu.

Soma, Fikiria, kisha Ujibu:

•Huduma ya kutia moyo ya Yohana Mbatizaji inatambulishwa katika toleo la kwanza la Luka. Linganisha maneno ya Yohana Mbatizaji katika Luka 3:16-18 na maneno ya Yesu katika Matendo ya Mitume 1:4-5. Unatambua nini?

• Pitia Matendo ya Mitume 1:6-8. Wanafunzi wanataka Yesu awafanyie watu wao walio Israeli kit gani? Yesu anajibuje? Anataka wajue na kufanya nini huku wakisubiri wakati wa Mungu? Ni kipi unachotaka Yesu akufanyie wewe na jamii yako, na jibu la Yesu kwa wanafunzi linazungumza nawe vipi leo?

• Karne nyingi kabla ya maelezo ya Luka kuhusu kupaa kwa Yesu kwenda mbinguni, nabii Danieli aliona maono kuhusu mfalme wa siku zijazo wa Israeli. Tazama maelezo ya kale kuhusu alichoona Danieli (tazama Danieli 7:13-14) na uyalinganishe na maelezo ya Luka (tazama Matendo ya Mitume 1:9-11). Unaona nini, na hili ni muhimu vipi?

• Acha mawazo yako yachochee maombi. Dhihirisha shukrani zako kwa Yesu. Mwambie unakotaka kuona urejesho wake katika maisha yako na jamii, na muombe ujasiri wa kupokea uwezo wa Roho wake, ili uweze kujiunga na mipango yake ya urejesho leo.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

BibleProject ilibuni Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarajio Sehemu ya 2 ili kuwatia watu moyo, vikundi vidogo, na familia mbali mbali waweze kusoma Matendo ya Mitume kwa siku 20. Mpango huu unajumuisha video za katuni, mihtasari yenye mawazo yanayojenga, na maswali ya tafakari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu na kuzama kwenye ubunifu wa fasihi wa mwandishi na kuelewa na kujifunza kutoka kwenye mtiririko wa mawazo yake.

More

Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com

Mipango inayo husiana