Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022Mfano
Wewe nena mambo yapasayo mafundisho yenye uzima(m.1). Tafsiri nzuri zaidi ni "mafundisho bora" au "mafundisho safi". Tito hatakiwi tu kukemea maisha mabaya na mafundisho ya uongo, lakini zaidi sanaafundishe ukweli wa neno la Mungu, ukweli wa Injili(m.5b). Awape Wakristo msimamo mpya, awape mafundisho bora, yeye mwenyeweakilishikalile neno la imani vile vile kama alivyofundishwa. Hivyo atawashinda wenye kupinga kama ilivyoandikwa katika 1:9. Nasi tufuate agizo hili katika kanisa letu! Fundisho bora la somo la leo lahusu mwenendo unaofaa kwa wazee wa kiume na wa kike na kwa wanawake vijana.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Aprili pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Tito. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/