Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022Mfano
Akamgusa sikio, akamponya(m.51). Tusemeje juu ya tendo la Yesu? Anawaambia mitume wake wasimtetee kwa upanga, na anamhurumia adui na kumponya! Ni upendo wa ajabu! Pia inatuonyesha kwamba Yesu baada ya kuomba amepata nguvu. Amepata uhakika kwa Mungu Baba kwamba lazima aende njia hii. Bila hivyo hakuna binadamu hata mmoja atakayeokolewa(Mt 26:52-54,Ndipo Yesu akamwambia, Rudisha upanga wako mahali pake, maana wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga. Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?Yatatimizwaje basi maandiko, ya kwamba hivyo ndivyo vilivyopasa kujiri?). Yesu amekubali kabisa kwa moyo wote. Anakwenda kwa hiari.Hii ndiyo saa yenu(m.53). Mpaka sasa hawajaweza kumkamata kutokana na ulinzi wa Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Aprili pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Tito. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/