BibleProject | Hekima ya MithaliMfano
![BibleProject | Hekima ya Mithali](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans-staging%2F32818%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Sura ya 12: Wenye Busara Hufunzika
"Yeyote anayependa nidhamu hupenda maarifa, lakini yeyote achukiaye kukosolewa ni mpumbavu." Kuanzia mstari wa kwanza, sura ya 12 imejaa kauli za ulinganifu: "Lakini hii, lakini ile—lakini lakini lakini!" Karibu kila mithali ni ya kutofautisha (isipokuwa mbili, tazama hapa chini). Huu ni mtindo mwafaka wa kufundisha, kwa kuwa tunapolinganisha mambo yaliyo kinyume, tunaweza kuona wazi tofauti zao na kufanya uamuzi unaofaa.
Mpangilio wa sura hii unakuwezesha kufanya uamuzi hasa unaohusiana na maneno yako na jinsi unavyowachukulia watu.
Wakati mwingine huenda mithali zikaonekana hazina mpangilio, lakini ukichunguza vizuri utaona utaratibu mzuri wa kipekee. Katika sura ya 12 kuna mithali 28, zilizogawanywa katika sehemu mbili zenye mithali 14 kwa kila upande.
Zimegawanywa kama ifuatavyo:
Sehemu ya 1
•Mstari wa 1 - Mtu mwenye busara hufunzika
•Mstari wa 2-13 - Zinalinganisha mithali 12 zinazohusu Maneno na Matendo
•Mstari wa 14 - Hitimisho lisilo linganifu
Sehemu ya 2
•Mstari wa 15 - Mtu mwenye busara hufunzika
•Mistari ya 16-27 - Zinalinganisha mithali 12 zinazohusu Maneno na Matendo
•Mstari wa 28 - Hitimisho lisilo linganifu
Mpangilio huu maalum unasaidia kuwasilisha ujumbe. Wenye haki hufunzika na huwa waangalifu wa mambo wanayosema na wanayofanya. Katika kifungu cha 28, mstari wa mwisho unahitimisha kwa kuzungumzia uzima wa milele: "katika njia ya haki...hakuna kifo."
Unaposoma sura ya 12, mwombe Bwana uwezo wa kuishi kwa hekima inayotokana na mithali hizi kupitia maneno na matendo yako.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![BibleProject | Hekima ya Mithali](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans-staging%2F32818%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.
More
Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com/swahili