Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022

SIKU 15 YA 30

Labda waliohubiri uongo hawakuhubiri sheria nzima. Walidai vitu vichache tu, hasa tohara. Lakini kushika sehemu tu, na kuacha sehemu nyingine, haiwezekani. M.3 unaeleza vizuri, Tena namshuhudia kila mtu atahiriwaye, kwamba ni wajibu wake kuitimiza torati yote. Lazima ushike sheria nzima ili uhesabiwe haki au umshike Kristo ili uhesabiwe haki naye. Paulo anaweka wazi akisema, Nawaambia ninyi ya kwamba, mkitahiriwa, Kristo hatawafaidia neno.Tena namshuhudia kila mtu atahiriwaye, kwamba ni wajibu wake kuitimiza torati yote. Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema. ... Chachu kidogo huchachua donge zima (m.2-4 na 9). Sheria itumike vizuri! Katika mambo kadhaa ya sheria ya Wayahudi tunao uhuru, k.m. tohara (m.6a, Katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa), ila katika mambo mengine lazima hata sisi Wakristo tuyafuate ili kumtii Bwana wetu Yesu Kristo. Imani yetu hutenda kazi kwa upendo. Katika m.6b imeandikwa, Imani itendayo kazi kwa upendo.

siku 14siku 16

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022

Soma Biblia Kila Siku Septemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Septemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wagalatia na Hagai. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/