Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

SIKU 18 YA 31

Yesu alitumia kiu aliyokuwa nayo na maji aliyopewa kwa lengo la kuongea zaidi na yule mwanamke Msamaria. Alitaka kuanzia hapo azinduke na kujua kuwa kuna maji ya uzima ambayo ni Yesu peke yake anayeweza kuyatoa. Bado Yesu ana ‘kiu’ kuwapa watu maji ya uzima. Pengine anabisha katika mlango wa moyo wako sasa, akisema, Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami (Ufu 3:20). Yesu anafahamu dhambi, taabu na mahangaiko yako yote. Na sasa anataka kuingia kwako akupe furaha tele na amani tele hadi uzima wa milele. Tafakari zaidi maana ya neno la Yesu katika m.14, Ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele!

Andiko

siku 17siku 19

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

Soma Biblia Kila Siku Januari/2023 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mithali, Yohana na Malaki. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/