Kugeuka Kutoka Katika Masuala Ya MihemkoMfano
Acha nikukumbushe kweli yenye umuhimu sana kuhusu mihemko: Haina akili.
Hayafikirii. Mihemko hujibu tu. Mihemko ni lazima iazime mawazo kusudi ichochee hisia. Kwa hivyo, ye yote au cho chote kinachodhibiti mawazo yako, hudhibiti jinsi unavyojihisi. Mihemko yako huanzishwa na kutawaliwa na jinsi unavyofikiri kuhusu hali ya maisha yako. Kwa hivyo, ikiwa wataka kutawala mihemko yako na kushinda ngome za kimihemko katika maisha yako, unahitaji kudhibiti mawazo yako.
Unapopatanisha mawazo yako na kweli ya Mungu, utawekwa huru.
Angalia kwenye kioo. Huyo mtu unayemwona alisulubishwa, alizikwa na akafufuliwa pamoja na Kristo. Machoni pa Mungu, Yesu alipokufa miaka elfu mbili iliyopita, wewe pia ulikufa. Alipozikwa, ulilazwa naye kaburini. Alipofufuka, nawe ulifanya hivyo. Ingawa waweza kuwa umempokea Kristo muda mfupi uliopita, Mungu alichukuwa kilichompata Yesu miaka mingi iliyopita, na kukifanya kuwa sehemu ya ukweli wako wa kiroho.
Shetani ni mjuzi wa kupanda mawazo akilini mwako, na kukufanya ufikiri ni yako mwenyewe. Labda unamsikia akisema kitu kama hiki, “Siwezi kushinda kujithamini kwa chini na mtego wa kujilinganisha. Siwezi kuwa huru kutokana na utumwa huu wa kimihemko. Siwezi kushinda mazoea haya ya zamani ya kuingia katika hali ya huzuni.” Anaweza kusema mambo hayo kwako, au yawezekana umejisemea mwenyewe, Lakini ili ushinde, ni lazima uache kuamini uongo. Matamshi hayo yote yawezekana kwamba yalikuwa kweli wakati ambapo mtu wa kale alipokuwa hai, lakini mtu huyo alikufa msalabani pamoja na Kristo. Wewe ni kiumbe kipya kabisa (2 Wakorintho 5:17).
Ni uwongo gani unaamini juu yako mwenyewe?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Wakati ambapo maisha yako yanatoka katika upatanisho wa neno la Mungu, hakika ni kwamba, utakabiliwa na hali ngumu yenye matokeo yaletayo uchungu. Mihemko yako inapokosa kudhibitiwa nayo ikaanza kuamua ustawi wako, utajikuta umejifungia katika gereza la kujitengenezea ambalo linaweza kuwa vigumu kwako kutoroka. Wahitaji usawaziko, na kujifunza jinsi ya kumtumaini Mungu. Mruhusu Tony Evans akuonyeshe njia ya uhuru wa kimihemko.
More
Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/