Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yesu Mwalimu WetuMfano

Yesu Mwalimu Wetu

SIKU 3 YA 3

Mafundisho ya Yesu yanahitaji jibu. Kustaajabia tu Yesu kama Mwalimu mkuu, bila kutumia kweli alizofundisha, ni kupoteza hazina ambayo alizungumza juu yake. Pia ni kujiweka katika hatari ya dhoruba za maisha zinapokuja

Hapo awali nilitaja mahubiri ya Yesu ya Mlimani. Alimaliza mahubiri kwa hadithi fupi kuhusu watu wawili. Mtu mmoja alijenga nyumba yake juu ya mwamba, msingi imara; mtu mwingine alijenga nyumba yake juu ya mchanga. Hoja ya Yesu ni kwamba mtu anayetenda kulingana na mafundisho yake anajenga juu ya msingi ulio imara, lakini mtu ambaye anashindwa kutii maneno ya Yesu anajiweka katika hatari. Dhoruba huja katika maisha yetu yote. Kujenga maisha yetu juu ya msingi thabiti wa Yesu na mafundisho yake hutupatia uwezo wa kustahimili mashambulizi.

Acha niseme tena: Kustaajabia Yesu tu kama Mwalimu mkuu, bila kutumia kweli alizofundisha, ni kujiweka katika hatari ya dhoruba za maisha zinapokuja. Ni sawa na kutangaza kwamba humwamini hata kidogo. Utii kwa yale ambayo Yesu anafundisha ni uthibitisho kwamba unamwamini. Imani, katika hali zote, inapaswa kudhihirishwa, sio tu kujadiliwa.

Kuamini maneno ya Kristo kwa kutenda kunahitaji imani. Imani ni kitu ambacho mara nyingi tunakosa kuelewa. Tunaitambua kama hisia, kitu tunachoshikilia kiakili, au kitu tunachosema tunaamini. Hata hivyo, imani hupimwa kwa maisha yako, si midomo yako. Inahusisha miguu yako, si tu hisia zako. Inapaswa kuwa taratibu ya maisha, siyo tukio.

Kwa kweli, kutoishi kwa imani ni kumwita Mungu mwongo. Ni kupinga uadilifu wake kwa sababu imani inamaanisha kumchukua kwa neno lake. Imani ina nguvu tu kama kitu ambacho imeshikamana nayo. Unaweza kuwa na imani yote ulimwenguni kwamba gari lako lingeota mbawa ghafla na kukupeleka mwezini, lakini bado ungeishia chini. Hata hivyo unapoambatanisha imani yako kwa Yesu Kristo na Neno lake—na unajibu kwa kutii yale ambayo amefunua—hiyo ndiyo imani inayohamisha milima (Mt. 17:20). Kuitikia mafundisho ya Yesu inamaanisha kumwamini vya kutosha kufanya kile anachosema.

Hungeajiri mwalimu wa muziki, mtaalamu wa programu za kompyuta, au mtunza bustani ili akufundishe jinsi ya kufanya ustadi fulani kisha usitumie kile alichokuonyesha. Hiyo itakuwa ni kupoteza muda na pesa zako. Zaidi ya hayo, mtu ambaye alikwenda chuo kikuu kujifunza jinsi ya kuwa mhasibu, kwa mfano, lakini akachagua kutofuata sheria za hisabati na biashara hatachukuliwa kuwa mjinga tu, bali pia atakuwa hana kazi.

Yesu ndiye Mamlaka kuu ya jinsi twapaswa kuishi maisha yetu. Naye ametupa mafundisho yake katika Neno lake. Kuisoma, kujifunza, kuijadili, na kisha kutotekeleza haina maana hata kidogo. Inaleta maana kama vile kujenga nyumba yako juu ya mchanga. Sikiliza mafundisho ya Yesu na ujibu kwa utii wenye kutumainiwa.

Je! unawezaje kutumia mafundisho ya Yesu katika maisha yako ya kila siku?

Soma. Soma mojawapo ya Injili na unapokutana na mafundisho ya Yesu, tambua jinsi gani ya kuishi kulingana na mafundisho hayo kungenufaisha maisha yako.

Ahidi. Fanya uamuzi wa makusudi wa kuishi kulingana na mafundisho ya Yesu.

Fundisha. Fikiria kuongoza kikundi kidogo cha kujifunza Biblia au kufundisha na kufanya kazi na watoto au wanafunzi. Acha Mungu akutumie kuwasiliana na wengine mafundisho ya Yesu.

Keti miguuni pa Yesu. Jifunze kutoka Kwake. Na uishi maisha yako kwa ukamilifu.

Tunatumahi kuwa mpango huu ulikuhimiza. Kwa habari zaidi kuhusu wizara, bofya hapa.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Yesu Mwalimu Wetu

Wewe unaenda wapi kujifunza jinsi ya kuwa mtu bora au kushinda changamoto? Wewe unamtafuta nani akufunze lilo bora au jinsi ya kufanya maamuzi sahihi? Je! Unakwenda kwenye magazeti? Mtandao wa kijamii ya YouTube? Tony Evans anashiriki kuhusu Mtu Mkuu zaidi jinsi aweza kukufundisha kuhusu maisha naye ni Yesu Kristo. Hebu tuchunguze jinsi Mpaji wa uzima pia ni Mwalimu wa maisha.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/

Mipango inayo husiana