Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Gundua Kusudi LakoMfano

Gundua Kusudi Lako

SIKU 2 YA 5

Kuwa tayari kwa wito wako ni kama kwenda kwenye mkahawa wa kuuza chapati mesto, au pizzeria. Ninazungumza kuhusu mahali ambapo chapati mesto iliyo halisi hutengeneza papo hapo. Yote huanza na mpira wa unga. Wao hubiringisha unga ile, huku wakiikanda na kuiponda. Kisha huanza kuitwanga twanga. Baada ya kuiponda kwa muda, wanaanza kuirusha hewani na kuizungusha. Unga huo unapitia mengi ili mimi na wewe tupate raha ya kuula.

Lakini unapoenda kwenye pizzeria, hauulizi kupewa unga. Unataka vitu vizuri. Unataka mchuzi, jibini, na labda nyama au mboga juu. Kila mtu anataka vitu vyema, lakini huwezi kupata vitu vyema mpaka unga uwe umeandaliwa. Vivyo hivyo, mtu anapaswa kuwa tayari kwa wito wake. Wakati mwingine, maandalizi yetu huanza kwa kutwangwa na kupondwa. Wakati mwingine ina maana ya kurushwa rushwa pande zote au kupondwa kwa muda kidogo. Lakini hii ni katika maandalizi tu ya mambo mazuri.

Katika matuta na majeraha ya maisha, Mungu anakutayarisha kwa ajili ya hatima kamilifu aliyokuumba ili uishi nayo. Lakini jinsi unavyoitikia matuta na vidonda hivyo kunaweza kuathiri jinsi unavyofikia hatima yako kwa haraka. Ni rahisi kukata tamaa, kukubali kushindwa na kuondoka wakati ambapo changamoto za maisha zinaonekana kuwa hazina maana au chungu sana. Lakini ikiwa utayaweka macho yako kwenye kusudi, na sio maumivu, Mungu ataitumia kwa wema wako na utukufu wake. Anafanya mambo yote pamoja kwa wema unapompenda na kuishi kulingana na wito wako. Hakuna kitu kama maumivu ya yasiyo na maana au uzoefu wakati wewe ni mtoto wa Mfalme.

Weka macho yako kwenye makusudio - matokeo ya mwisho - na utapata nguvu kwa safari inayokupeleka huko. Una hatima tukufu ya kugundua na kutimiza.

Sala:

Baba uliye mbinguni, nikumbushe katika nyakati hizo, saa, siku, wiki, miezi au hata miaka ya maandalizi ya kwamba una mpango mzuri na kusudi la maisha yangu. Nipe neema ya kukuamini katika yote ili nisipoteze muda katika kujifunza na kurudia kujifunza tena masomo yale yale ninayohitaji kujua ili kwa ukamilifu niweze kutekeleza hatima yangu.

Andiko

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Gundua Kusudi Lako

Katika mpango huu wa kusoma kwa ufahamu, mchungaji na mwandishi mashuhuri Tony Evans anakupitisha katika mchakato wa kugundua kusudi lako.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/