Ndoa Ya UfalmeMfano
Msichana mdogo alikuwa akicheza na mikono ya nyanya yake siku moja kwa ghafula aliacha kucheza nayo, ili kuchunguza pete ya ndoa ya nyanya yake. Baada ya dakika chache, alimuuliza bibi yake kwa nini pete ilikuwa kubwa na nzito. Haikuwa kitu kama pete nyembamba zipendezazo zaidi kama alizoziona. Bibi huyo alitabasamu na kusema, “Kwa sababu nilipoolewa, pete zilitengenezwa ili kudumu.”
Sababu mojawapo ambayo wanandoa wengi hurudisha pete zao ni kwa sababu wanaona ndoa kama vile ni mkataba. Mkataba ni makubaliano yenye masharti kati ya watu wawili au zaidi kuashiria kwamba pande zote zitafanya jambo fulani. Mikataba hufanywa kwa muda mfupi na msingi ukiwa kwenye taarifa za "ikiwa, basi". "Ikiwa watafanya hivi, basi mimi nitafanya vile." Watu wanaingia kwenye mikataba kwa sababu ya kile watakachopata kutoka kwacho. Wakati wanapokosa kupokea kile wanachotaka, au ikiwa watapata chaguo bora zaidi, basi watahalalisha kuisitisha.
Hata hivyo, Biblia haielezei ndoa kwa njia hii, lakini inaifafanua kama agano. Agano ni kifungo cha kiungu kilichoundwa kufunganisha ikiwa na maana kwamba ni ya kudumu. Ina sheria, majukumu na faida. Maagano ni mahusiano ya dhati yanayoanzishwa kwa manufaa ya mtu mwingine. Ndani yake, wema wa uhusiano huchukua nafasi ya kwanza juu ya mahitaji ya mtu binafsi. Hii ndiyo sababu maagano hufanya ahadi zisizo na masharti. Kimsingi, ni pale Mungu anapofanya kitu rasmi katika ulimwengu wa kiroho ili mwanadamu aishi katika ulimwengu asilia. Katika hali zote, nadhiri za arusi hufanywa “mbele ya Mungu” na kwa hiyo pamoja na Mungu na pia pamoja na mwenzi wa ndoa. Kuvunja agano na mwenzi wako ni kulivunja na Mungu.
Wakati mume na mke wanaishi katika ndoa ya agano badala ya masharti ya mkataba, watapata kifuniko. Ni kama mwavuli. Mvua inaponyesha, mwavuli hauzuii mvua, lakini inazuia mvua kukunyeshea.
Kuishi chini ya kifuniko cha Mungu hakutazuia changamoto katika ndoa yako, lakini changamoto hizo hazitakuathiri kwa njia sawa na kama vile haungekuwa chini ya kifuniko chake.
Ni jinsi gani unawezaje kuanza kuhusiana na mwenzi wako kwa masharti ya agano?
Kuhusu Mpango huu
Ndoa huja na furaha nyingi na changamoto kubwa. Sababu mojawapo ya changamoto hizo ni kwa sababu tumesahau kusudi la kibiblia la ndoa. Tumemuondoa Mungu na kufafanua ndoa kwa msingi ya furaha. Lakini ndoa ipo ili kumtukuza Mungu kwa kupanua wigo Wake ulimwenguni kote. Katika mpango huu wa siku tano wa kusoma, Dkt. Tony Evans anakupeleka kwenye safari ya ndoa ya ufalme.
More
Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/