Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Fukuza HofuMfano

Fukuza Hofu

SIKU 2 YA 3

Unafanya nini wakati ambapo hofu inaanza kuzamisha mawazo yako na haikuwachilii kwenda?

Maandiko yanasema kwamba kiuasumu bora cha woga na wasiwasi ni maombi. Ili kuona kile kinachohusika katika maombi na kile ambacho maombi yanaweza kufanya dhidi ya hofu uliyo nayo, angalia Wafilipi 4:6–7. Aya wa 6 inasema hivi, “Msijisumbue kwa neno lolote, bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.”

Hofu inapokushika, anza kwa kupinga hofu hiyo kwa kweli wa Mungu. Mungu anasema lazima ubadilishe mtazamo wako kwa sababu ye yote au chochote kinachotawala akili yako, kinakutawala. Mungu hataki uzingatie mawazo yako ya kutisha na kutawaliwa nayo. Badala yake, Mungu anataka umzingatie yeye na kuruhusu Neno lake na Roho Wake akudhibiti. Hii ndio sababu ya maombi kuwa yenye umuhimu sana. Utaratibu hapa ni rahisi. Usiogope chochote, bali omba kuhusu kila kitu.

Wafilipi 4:6 hutumia neno la jumla kwa ajili ya maombi hususan neno lenye maana bayana, nalo ni “dua”, ambalo lina maana ya kuomba hususan jibu la hitaji fulani. Kimsingi hiyo ina maana kwamba unapaswa kufanya dua kuhusu kila kitu, iwe ombi lako ni la jumla au mahususi. Ikiwa una hofu inayokusumbua lakini hauonekani kubainisha ni nini, ichukue kwa Bwana katika maombi—Yeye anajua ni nini. Au ikiwa una hofu fulani ambayo unaweza kuona wazi wazi akilini mwako, ipeleke kwake pia. Mwombe akusaidie kuondoa hofu zako na kuzibadilisha na ukweli wake, kisha umshukuru kwa imani kwa kukufanyia hivyo.

Bwana mwenye neema, Je! Shomoro wawili hawauzwi kwa senti moja? Na bado unajua kila kitu kinachotokea kwao. Umehesabu pia nywele za kichwa changu. Nisaidie kupata ujasiri wa kujua jinsi unavyonijua na kunipenda. Nikumbushe leo kwamba sihitaji kuogopa, kwa sababu wewe ndiye mwenye udhibiti wa vitu vyote na umeahidi kutoniacha wala kunipungukia. Asante kwa ahadi zako, ambazo huniletea amani. Katika jina la Kristo. Amina.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Fukuza Hofu

Unaweza kushinda hisia za hofu. Dkt. Tony Evans anakuongoza kwenye njia ya uhuru katika mpango huu wa usomaji wa kupata ufahamu. Gundua maisha ya furaha na amani ambayo umekuwa ukitaka, unapotumia kanuni zilizowekwa katika mpango huu.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative