Kuomboleza VyemaMfano
Kwa miaka mingi sasa, kumekuwa na mawazo yenye msimamo mkali katika kanisa la Kikristo kuhusu imani, jinsi ya kuifanyiza kazi na nini cha kutarajia kutoka kwa Mungu Mkuu unapofanya hivyo. Wengine wanapendekeza kwamba unahitaji kukiri kwa uhakika kile unachotaka kutoka kwa Mungu (kuondolewa kwa magonjwa, usalama wa kudumu, kutokuwepo na hasara, nk.) na kuamini kwa moyo wako wote kwa ajili haya, na atakupa chochote unachoomba. Wengine wameonyesha imani kwa njia hiyo kwa wapendwa wao waliokuwa wagonjwa, na kutazama tu ugonjwa huo ukiwadai katika kifo. Kwa hiyo, je, imani yao ilikuwa dhaifu sana? Hapana.
Ingawa sisi sote tumeitwa kuwa na ujasiri katika imani yetu, lazima pia tusawazishe hilo na maarifa kwamba tunamtumikia Mungu Mkuu, Ambaye wakati fulani mapenzi yake kuwahusu watu tunaowapenda ni kwamba waondoke duniani. Hatuwezi kumtawala Mungu. Imani ina maana kwamba tunapaswa kuamini hata wakati tunapokabili maumivu na hasara. Ni lazima tushiriki katika mchakato wa kuomboleza ili wale ambao wanabaki katika maisha yetu wakati wangali hapa duniani bado waweze kupatika njia ya kuingia katika mioyo yetu na afya, upendo na zawadi. Ni lazima tuomboleze vyema sio tu kwa ajili yetu wenyewe na kwa uponyaji wetu tu, ila na kwa ajili ya wapendwa wetu wengine wanaotuhitaji na wanaotaka tuwe pamoja nao.
SALA:Bwana, tia nguvu imani yangu ili nipate ujasiri wa kukuomba yale unayonitakia. Nikumbushe kwamba wewe si Mungu ninayeweza kuendesha au kudhibiti, lakini ni Mungu ninayeweza kumkaribia. Nipe moyo wa kuamini kwamba kile ambacho kimetokea katika majonzi haya chaweza kuwa na manufaa zaidi kwako na mapenzi yako kwa maisha yangu. Ninakushukuru kwa uwepo wako na uaminifu wako katika maisha yangu. Sasa hivi, ninakuja Kwako nikiomba kwamba uimimine Roho wako juu yangu. Endelea kunitia nguvu ninapolazimika kubeba uzito mkubwa wa majonzi. Ninaomba kwamba unipe amani isiyo ya kawaida. Niepushe na kuishikilia huzuni yangu ndani au kuiruhusu iamuru jinsi ninavyoishi maisha yangu ya siku baada ya siku. Nisaidie kushughulikia msiba wangu kama mchakato, ambapo ninaweza kuomboleza na kupona vyema. Katika mambo yote, niyatoa mapenzi yangu kwako, moyo wangu kwa wako, na kutumaini kwamba nijapopita katika bonde la mauti, Wewe kwa kweli uko pamoja nami, ukiniongoza na kunifariji. Katika jina la Kristo, amina.
Tunatumai kuwa mpango huu umekuhimiza. Ili ujue zaid kuhusu huduma ya Tony Evans, bofya hapa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Huzuni huja kama sehemu ya asili ya maisha. Unapompoteza mtu unayempenda, inaweza kuwa vigumu kujiongoza katika mchakato wa kuomboleza. Kupitia mpango huu wa kusoma, Tony Evans anazungumza kutoka moyoni mwake kulingana na jinsi alivyompoteza kwa ghafla mpwa wake wa kike. Kanuni hizi zinaweza kukusaidia kujifunza jinsi ya kuomboleza vyema na kukumbatia uponyaji.
More
Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative