Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023Mfano
Israeli na Yuda walipigwa na mataifa adui kwa sababu ya dhambi yao. Lakini kumbe, hata hao maadui watahukumiwa na Mungu, ijapokuwa aliwatumia kuwa fimbo kwa taifa lake. Tunaonywa tusikose unyenyekevu na huruma, maana kama ulivyotenda, ndivyo utakavyotendwa (m.15). Tukijitukuza, Mungu atatudhili kwa aibu na kilio. Lakini tukimtegemea, Mungu atatuokoa. Kwa ufahamu zaidi linganisha m.17 unaosema, Katika mlima Sayuni watakuwako wenye kuokoka, nao utakuwa mtakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki milki zao. Maana haikosi siku ya Bwana itakuja, na hapo itaonekana kwamba ufalme pamoja na nguvu na utukufu ni wa Bwana, hata milele. Amina!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Februari 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Warumi na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/