Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Amani Ya KristoMfano

Amani Ya Kristo

SIKU 3 YA 3

Umewahi kuruka ndani ya ndege katikati ya dhoruba? Nimewahi. Vikombe vilianguka vinywaji vilimwagika, vyumba vya juu vilipasuka, na watu waliokuwawamenizunguka pande zote wakapiga mayowe. Sijawahi kuwa mtu wa kuogopa kuruka, lakini nyakati hizo hata walio dhaifu kati yetu hujifunga mkanda na kuwa makini.

Hadithi inasimuliwa juu ya safari ya ndege ambayo ilikumbana na mtikisiko usio wa kawaida, uliotupa ndege upande kwa upande katika dhoruba kali za upepo. Mawingu yalionekana kuwa meusi zaidi kama makaa ya mawe. Radi ilipiga karibu. Kimya cha kutisha kilitanda juu ya abiria waliokuwa katikati ya sauti kuu zilizojaa woga, hofu na mayowe yao. Hakuna aliyejisikia salama.

Isipokuwa kwa mtoto mmoja mdogo. Alikaa pale akiwa amejishughulisha na daftari na kalamu yake, akichora picha yake akipanda mti kwenye siku iliyoangaa kwa mwanga wa jua. Ungelimtazama, usingeweza kudhani alikuwa kwenye ndege katikati ya dhoruba. Abiria mmoja aliyekuwa karibu alimwona na kujiuliza jinsi angeweza kuhisi mtulivu hivyo, kwa hivyo akamuuliza mvulana huyo mchanga, “Je, huogopi?”

Alitazama tu kutoka kwenye karatasi yake kwa muda, akatabasamu, na kusema, “Hapana.”

"Kwa nini isiwe hivyo?" yule bibi alipeleleza, vidole vikishika kiti chake kwa nguvu.

"Kwa sababu baba yangu ndiye rubani," alijibu kwa uhakika tena kwa ufahamu kuwa ni jambo la ukweli kisha akarudi kwenye mchoro wake.

Wakati mwingine maisha yanaonekana kutodhibitiwa, lakini kujua ni nani aliye katika usukani kunafaa kuleta moyo wa amani.

Neno amani hutumika sana, lakini mara nyingi hatuelewi maana yake halisi.

  • Katika Mashariki ya Kati, amani inawakilisha kitu kama vile makubaliano ya kuleta ahueni ya muda kutokana na vita.
  • Kwa mama mdogo, inaweza kusimama kwa saa hiyo wakati watoto wachanga wanalala.

Amani ina maana tofauti kwa watu tofauti.

Amani ambayo Yesu hutoa haifanani na nyingine. Amani yake huzaa utulivu wa ndani katikati ya machafuko ya nje. Tunapata amani yake tunapofanya badilishana naye hofu zetu za dhoruba kwa kicho chake chenye afya na heshima kwake. Tunapohamisha macho yetu kutoka baharini hadi kwa Mwokozi, amani hutokea.

Paulo alituambia tuitikie amani ya Mungu kama vile tufani ilimjibu Yesu usiku ule kwenye Bahari ya Galilaya. “Na amani ya Kristo … itawale mioyo yenu” (Wakolosai. 3:15). Neno la Kigiriki linalotumiwa kwa ajili ya kudhibiti linamaanisha “uamuzi.” Sote tunajua mwamuzi hufanya nini. Anatangaza jinsi mambo yalivyo. Chochote anachosema— mpira unaelekea wapi, goli, kutoka nje, au lolote lile — ndivyo ilivyo.

Vivyo hivyo, chochote Yesu anachosema kuhusu jambo, ndivyo kilivyo. Imekwisha. Hivyo anaposema “Jipeni moyo! Mimi nimeushinda ulimwengu” (Yohana 16:33), imekwisha … na tunapaswa kujibu ipasavyo—kwa ujasiri.

Ulimwengu wako unaweza kuwa unasambaratika, lakini sio lazima usambaratike pamoja nao. Huwezi kudhibiti kila wakati kile kinachokupata au dhoruba ambazo unaweza kuruka ndani yake, lakini una uwezo wa kudhibiti jinsi unavyoitikia. Kuitikia uwepo na nguvu za Yesu maishani mwako hukuwezesha kuacha woga wako na badala yake kuweka amani—amani yake. Haimaanishi kuwa hutakuwa na matatizo, lakini ina maana matatizo yako hayatakumiliki wewe.

Mahusiano yanaweza kudhoofika. Ajira zinaweza kukoma. Afya inaweza kudhoofika. Uchumi unaweza kuendelea kudorora na kugeuka. Lakini Yesu anasema, “Nyamaza! Tulia!" Unaweza kutulia kwa faraja kwenye mto wako, kwa maana amekuweka mikononi Mwake.

Tunatumai kuwa mpango huu umekuhimiza. Ili ujue zaid kuhusu huduma ya Tony Evans, bofya hapa.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Amani Ya Kristo

Tunaweza kutarajia siku mbaya. Siku hizo huja kwa wanaoishi katika dunia iliyoanguka na ubinadamu ulioanguka. Kwa kweli, amani ingekuwa bidhaa adimu ikiwa tungetegemea hali zetu kama chanzo pekee cha amani hiyo. Ila bado tuna chanzo bora zaidi cha amani ... na ujasiri. Kwa kweli, ndicho chanzo pekee cha kweli: Yesu.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/

Mipango inayo husiana