Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Faraja Ya Majaliwa Ya MunguMfano

Faraja Ya Majaliwa Ya Mungu

SIKU 2 YA 3

Moja ya sifa kuu za kitheolojia za Mungu ni ukuu wake. Ukuu unarejelea tu utawala Wake juu ya viumbe Vyake vyote. Kulingana na Waefeso 1:11, Yeye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake mwenyewe. Katika Warumi 11:36 tunasoma, “Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, na kwa njia yake, na vya kwake yeye…”

Hakuna kitu kinachoepuka utawala na ushawishi wake. Mungu ndiye mtawala wa kila kitu kwa sababu yeye ndiye aliyeumba na kuhimili kila kitu.

Kuelewa ufalme wake hutupatia alama zinazoongoza safari yetu katika eneo la majaliwa yake Mungu. Lakini ili kuelewa utawala wa Mungu, ni lazima kwanza tuelewe kile anachotawala: ufalme wake.

Sasa, ikiwa wewe ni Mmarekani, kuna uwezekano mkubwa wewe ni Mmarekani kwa sababu ulizaliwa hapa. Ikiwa wewe ni sehemu ya ufalme wa Mungu, ni kwa sababu umezaliwa mara ya pili katika ufalme wake. Sababu inayokupasa usitake kukosa ufahamu kamili wa ufalme unapotafuta kuelewa majaliwa na ukuu sio tu kwa sababu inaathiri kuelewa kwako wa mambo haya mawili tu, lakini pia ni ufunguo wa kuelewa Biblia nzima. Mada kuu iliyokitovu kinachounganisha Biblia yote ni utukufu wa Mungu na maendeleo ya ufalme wake. Uzi unaoungana kutoka Mwanzo hadi Ufunuo—tangu mwanzo hadi mwisho—unalenga jambo moja: utukufu wa Mungu kupitia kuendeleza ufalme wa Mungu.

Wakati unapokosa kuelewa mada hiyo, basi Biblia inakuwa hadithi zisizounganishwa ambazo ni nzuri kwa uvuvio lakini zinaonekana kuwa hazihusiani katika kusudi na mwelekeo. Biblia ipo ili kushiriki harakati za Mungu katika historia kuelekea kuhusu kuthibitshwa na kupanuliwa kwa ufalme wake. Kuelewa hilo kunaongeza umuhimu wa hati hii ya miaka elfu kadhaa na uhusiano kwa maisha yako ya kila siku, kwa sababu ufalme hauko wakati huo tu; ni sasa.

Kote katika Biblia, ufalme wa Mungu ni utawala wake, mpango wake, taratibu yake. Ufalme wa Mungu unajumuisha yote. Inashughulikia kila kitu katika ulimwengu. Kwa kweli, tunaweza kufafanua ufalme kama utawala kamili wa Mungu juu ya viumbe vyote. Ni utawala wa Mungu ndio wenye umuhimu mkuu na sio utawala wa mwanadamu.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Faraja Ya Majaliwa Ya Mungu

Maisha yana namna ya kukufanya ujisikie kana kwamba umesahaulika. Iwe ni wakati maisha yanapoanza kugeuka kuwa mabaya au wakati mambo yanaonekana hayaendi sawa, Mungu ana mpango na wewe. Katika mpango huu wa siku 3, Tony Evans anafundisha jinsi Mungu anavyodhibiti kila kitu, haijalishi kinaonekana kibaya kiasi gani.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/