Njia Ya Mungu Ya MafanikioMfano
Watu wengi hawaoni mafanikio jinsi yalivyo. Wanatafuta fataki, kujionyesha kupita kiasi lakini kwa juujuu tu na uwanja mmoja mkubwa wa kupigiwa makofi. Sekta yetu ya burudani na tovuti, na mitandao ya kijamii, pamoja na michezo ya kitaaluma, zimeunda mtazamo usio halisi wa maana ya kuwa mtu aliyefanikiwa. Kwa bahati mbaya, matarajio haya yasiyo ya kweli mara nyingi hutufanya tukose mafanikio ya kweli yanapokuja. Au inatufanya tukose kufurahia mafanikio tuliyoyapata. Kwa sababu ya kutotambua matokeo yaliyoko, tunaweza kuishia kukimbiza jambo kubwa lingine linalofuata. Na kisha lifuatalo, na baada ya hapo tena lifuatalo. Tunajikuta tunazungusha magurudumu yetu katika mbio za maisha za panya – mbio zisizokuwa na mwisho.
Kwa kuwa tunaishi katika ulimwengu uliovunjika, uliochafuliwa na dhambi na athari zake, hatua nyingi za mafanikio katika maisha yetu zinaweza kuonekana kuwa na ladha kuwili, tamu na chungu wakati ambapo yote yamesemwa na kufanywa. Isipokuwa tuelewe asili ya mafanikio ya kiroho, tunaweza kumalizia katika jitihada zisizoisha za kitu ambacho tayari tumepewa. Bila ufahamu dhahiri wa mafanikio ya ufalme, hatutajua jinsi ya kuwekeza wakati wetu, talanta na hazina zetu. Chochote unachopanda ndicho kitaamua uvunacho. Lakini mara nyingi Shetani hutufanya tupande katika mambo yasiyofaa kwa sababu hatuelewi jinsi mafanikio ya kweli yanavyoonekana.
Je, ni mambo gani matatu makuu au maono ambayo umepanda ndani kwa miaka michache iliyopita?
Je, umepata mavuno yapi, na je, yanafaa katika ajenda ya ufalme wa Mungu?
Kuhusu Mpango huu
Kila mtu anatafuta mafanikio, lakini wengi hawayapati kwa sababu wanachofuata ni ufahamu potofu wa nini maana ya kuishi maisha ya mafanikio. Ili kupata mafanikio ya kweli unahitaji kuweka macho yako katika ufafanuzi wa Mungu wa maana yake. Mruhusu mwandishi wa vitabu vinavyouzwa sana Tony Evans akuonyeshe njia ya mafanikio ya kweli ya ufalme na jinsi unavyoweza kuipata.
More
Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/