Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mimi Niko Aliye MkuuMfano

Mimi Niko Aliye Mkuu

SIKU 3 YA 3

Jina “Mimi Ndimi” katika theolojia linaitwa tetragramatoni. Hiyo ni kauli ya kitheolojia inayomaanisha tu: Herufi nne. Mimi Ndimi inaundwa kwa herufi nne katika lugha ya Kiebrania nazo si vokali. Hapo awali, lugha ya Kiebrania iliandikwa katika abjad (aina ya maandishi ya ishara), kumaanisha kuwa haikuwa na vokali zozote. Kwa kuwa jina hili halina vokali, halikuweza kutamkwa. Hii ni kwa sababu hakuna njia ya kukariri konsonanti nne kama neno lenyewe.

Pia, katika dini ya Kiyahudi, jina hilo lilionwa kuwa takatifu sana haliwezi kusemwa. Hivyo, ili kuzungumza juu ya Mungu, walichofanya siku hiyo ni kuchukua vokali kutoka katika lugha ya Kiebrania na kuziingiza katika jina hili YHWH. Hii ikawa Yahweh katika muundo wa maandishi. Baadhi ya Wayahudi walifanya kitendo cha kubadilisha jina lililosemwa na Adonai walipokuwa wakizungumza katika sinagogi kwani walihisi jina Yehova lenyewe lilikuwa takatifu sana kuweza kusemwa. Hii bado inafanywa na wengi hadi leo. Tunaijua kuwa Yehova katika lugha yetu ya Kiingereza. Katika Maandiko, jina hili mara nyingi huandikwa kama BWANA yote katika herufi kubwa. Maana ya jina hili ni kwamba, Mungu adumushiye agano na mahusiano.

Tunapochambua utungaji wa jina hili Mimi Ndimi, tunapata kuangalia kwa karibu zaidi moyo wa Mungu. Hili ni jina la uhusiano wa Mungu. Inaashiria tabia Yake ya uaminifu, ya kuweka maagano. Neno la kwanza katika jina hili ni "Mimi" na mimi ni kiwakilishi cha kibinafsi. Hii inatuambia kwamba ni Yeye anayezungumza na katika kujiita kwa jina hili, anaonyesha kwamba anataka kuwa na uhusiano nasi kibinafsi. Mungu hapendezwi tu na kuwa Mwenyezi, mwenye nguvu na mamlaka aliyeko huko juu. Yeye pia anataka kuzungumza nasi hapa chini tunapoishi. Kwa maneno mengine, tunaweza kuwasiliana naye kibinafsi.

Sio tu kwamba jina hili ni la kibinafsi, lakini pia linashiria wakati uliopo. "Niko" ni wakati uliopo. Haijapita (ilikuwa) wala si yajayo (itakuwa.) Jambo hili linatufafanulia kwamba Mungu hana wakati uliopita na hana wakati ujao. Hana jana na hana kesho. Kila kitu kuhusu Mungu ni SASA. Yeye tu NI.

Hivyo, Yesu aliposema, “Mimi Ndiye,” Aliwajulisha kwamba Yeye ni Mungu wa kibinafsi, aliyepo, mwenye nguvu, asiyeyumba, na anayejidhibiti.

Tunatumai kuwa mpango huu umekuhimiza. Ili ujue zaid kuhusu huduma ya Tony Evans, bofya hapa.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Mimi Niko Aliye Mkuu

Siyo tu kwamba jina la Mungu ni tangazo, lakini ni mojawapo ya majina yenye nguvu zaidi ya Yesu. Katika mpango huu wa kusoma, Dk. Tony Evans anafundisha kuhusu jina hili lenye nguvu na maana yake kwetu kama waumini.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/