Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023

SIKU 13 YA 30

Asali ni chakula na dawa muhimu. Kila mtu anaipenda. Kama mtoto ashauriwavyo kuipenda na kuila asali, vivyo hivyo na mwana wa Mungu, anatakiwa kulipenda Neno la Mungu lililo asili ya ubora wa maisha. Hekima ya Mungu ni Kristo. Ukimfuata huyu, utafurahia ukweli na kuwapenda watu, na utajifunza jinsi ya kuwatendea mema wabaya wako. Neno la Mungu linafundisha kuwa usifurahie kuanguka kwa watu wabaya (m.17 Usifurahi, adui yako aangukapo; Wala moyo wako usishangilie ajikwaapo), bali umwachie Mungu kulipa kisasi, maana ndiye mwamuzi sahihi. Yeye anasema, Kisasi ni changu mimi, na kulipa, Wakati itakapoteleza miguu yao; Maana siku ya msiba wao imekaribia, Na mambo yatakayowapata yatafanya haraka (Kum 32:35).

siku 12siku 14

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023

Soma Biblia Kila Siku/Aprili 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Yohana, Mithali na Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipango inayo husiana