Kristo, Malkia Wetu Esta HalisiMfano
Siku ya Kwanza – Ibada
Mimi na familia yangu tulienda likizo katika kituo cha mapumuziko huko mwambao wa pwani, Mombasa, Kenya. Mimi siwezi kuogelea, lakini kwa sababu nisiyoielewa, asubuhi moja niliamua kuruka katika bwawa la kuogelea. Kosa kubwa! Mara moja nilianza kuzama majini. Kwa bahati nzuri mmoja wa wanangu alihisi hali yangu ya hatari na kwa kitendo cha kishujaa alipiga mbizi ndani na kuniokoa.
Mtu anayezama majini kama nilivyozama hahitaji funzo la jinsi ya kutozama kwa yule anayesimama salama salmin katika ukingo wa bwawa hilo. La. Mtu aliyeloweka na kuzama maji anahitaji mtu ambaye anapoona ukosefu wa uwezo wa kujiokoa kwa yule azamaye, ajibainishe na hali mbaya ya mtu yule, na kupiga mbizi mara moja ili kuingilia katikati ya ile hali mbaya ya anayezama na kumvuruta yule mtu hadi mahali pa usalama.
Huo ndio usimulizi wa kitabu cha Esta katika biblia. Hadithi ya Esta inasisimua jinsi ilivyo sambamba na vile injili ya Yesu Kristo inavyotukomboa kiroho.
Kwanza, kitabu hiki kinatuonyesha udhaifu wetu na ukosefu wa tumaini la kujiepusha na dhambi na mauti. Pili, kinatukumbusha jinsi Kristo alijitambulisha nasi alipojivika mwili. Tatu, kitabu hiki kinaonyesha jinsi Kristo kwa kifo chake alishinda kifo na alipofufuka alitushindia uzima wa milele.
Leo tutaangazia ukweli wa kwanza: kwamba tunazaliwa ulimwenguni huu uliotandikwa na urithi wa kifo au mauti na hatuwezi kujiokoa au kuugeuza urithi huo.
Matukio ya kitabu cha Esta yalitokea katika mji mkuu wa Ufalme wa Uajemi. Ufalme huo ndio uliokuwa wa nguvu kuu nyakati hizo, Mfalme Ahasuero ambaye alimiliki toka Bara Hindi mpaka Kushi, juu ya majimbo ishirini na saba, na kiti chake kilikuwa huko Shushani ngomeni alipokuwa mtawala. Wakati huo, wayahudi walikuwa wamefukuzwa nchini mwao na kusambaratika uhamishoni katika eneo lote la miliki ya Uajemi.
La kustaajabisha ni kwamba kitabu cha Esta ndicho kitabu pekee katika biblia nzima ambapo jina la Mungu halijatajwa. Wala ombi. Lakini tunaona ukuu wa mwenyezi Mungu ukifanya kazi bila shauku katika matukio ya kitaifa yaliyounda historia ya ulinzi na utetezi wa Mungu kwa watu wake.
Kutoka mwanzo hadi mwisho, kitabu cha Esta kinasisimua mno. Sura ya kwanza, Malkia Vashti aondolewa madarakani alipokataa kuonyeshwa katika karamu ya hadhara ya mume wake Mfalme Ahasuero na wafanya kazi wake na waume wenzake. Sura ya pili, tunakutana na Esta, aliyekuwa yatima na binamu wake mkubwa Mordekai ambaye ndiye aliyemlea. Hawa walikuwa wazao wa kiyahudi waliokamatwa na kuwekwa uhamishoni na chini ya utawala wa Kiajemi zama hizo miaka mia moja iliyopita. Esta anachaguliwa kuwa mmojawapo wa wanawali ambao walipewa fursa ya kuania mbadilisho wa kiti cha malkia Vashti. Mfalme anamfadhili Esta na kumvisha taji la umalkia.
Iliyofuata ni Hamani bin Hamedatha ambaye kupandishwa cheo kama Makamu wa Rais na ambaye anashurutisha kila mtu kumsujudia. Isipokuwa, Mordekai hakuinama wala kumsujudia Hamani. Hamani anapandwa na hasira. Anaamua sio kumuua Mordekai pekee tu, bali wayahudi wote waliokuwemo popote katika eneo la Kiajemi.
Hadi mwisho mwa sura ya tatu wa kitabu cha Esta, wayahudi hawakuwa na lolote la kufanya kujiokoa na janga lililowakumba kutokana na chuki ya Hamani. Hadi mwisho mwa sura ya tatu ya kitabu cha Mwanzo, nasi pia tupo katika hali hiyo hiyo ya kutoweza kujiokoa na janga la dhambi. Sote huwa tunazaliwa tukiwa na upungufu wa utukufu wa Mungu na tunastahili kifo (Warumi 3:23, 6:23), hatuwezi kufanya chochote kuhusu hali yetu ya kiroho. Kama vile wayahudi wa nyakati za Esta, nasi pia tunahitaji Mwokozi atakaye zama majini ili atuokoe na atupatanishe na mungu. Ahsante Bwana: Kristo alikuja!
Kuhusu Mpango huu
Kitabu cha Esta ni hadithi ya kushangaza ya ujasiri na upendo ambayo inatuelekeza kwenye hadithi ya Yesu. Katika mpango huu wa siku tatu, Dk. Kwasi Amoafo anachunguza jinsi hadithi ya Agano la Kale ya Esta inavyofanana na injili na ni picha ya kushangaza ya ukombozi wetu wa kiroho kupitia Yesu, ambaye alijitambulisha pamoja nasi, aliingilia kati kwa ajili yetu, na kutuokoa tulipokuwa hatuna uwezo. ili kujiokoa.
More
Tungependa kuwashukuru Emmanuel Kwasi Amoafo kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://returningtothegospel.com/