Soma Biblia Kila Siku 02/2024Mfano
Mungu anapenda watu wake wakutane naye. Na kwa kuwa Yeye ni Mtakatifu, anamtuma Musa awaandae kwa kuwatakasa ili wakutane na Mungu. Watu wanatakiwa wajiandae kimwili na kiroho. Walimwitikia Mungu kwa kujitenga mbali na dhambi na mazoea ya kawaida ili wajitoe kwa Mungu. Mungu anawapenda na kuwapa heri watu wake. Ndiyo maana anawaandaa kabla hajakutana nao. Je, ni nini kinachotuandaa na kututakasa sisi ili kukutana na Mungu Mtakatifu? Yesu akijifananisha na mzabibu wa kweli, anasema juu ya wote walio kama matawi ndani yake,Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia(Yn 15:3). Roho Mtakatifu ndiye anayetutakasa kwa neno lake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 02/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/