Soma Biblia Kila Siku 10/2024Mfano
Katika historia ya wokovu, Mungu alimtoa mwanawe kuwa dhabihu iliyo bora zaidi ya zote zilizotangulia kutolewa. Hapana jambo jingine liwezalo kutusaidia kama tusipoijali dhabihu hiyo na kuacha kuupokea wokovu wa Yesu. Maana tutapata wapi dhabihu nyingine ya kuondoa dhambi zetu na kutupatanisha na Mungu? Imebaki hukumu ya kutisha tu.Twamjua yeye aliyesema, Kupatiliza kisasi ni juu yangu, mimi nitalipa. Na tena, Bwana atawahukumu watu wake. Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai(m.30-31). Maana tumeshasoma katika m.26 kwambatukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi. Lakini yule anayetaka kuiacha dhambi aliyotenda na kumtafuta Yesu ili asamehewe na kukubaliwa kuishi naye, asiogope kwamba amefanya dhambi kusudi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 10/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania, Kutoka na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz