Matokeo ya utafutaji
Efe 4:26 (SUV)
Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka;
Yak 1:19 (SUV)
Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;
Yak 1:20 (SUV)
kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki ya Mungu.
Efe 4:31 (SUV)
Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya;
Mit 19:11 (SUV)
Busara ya mtu huiahirisha hasira yake; Nayo ni fahari yake kusamehe makosa.
Mt 5:22 (SUV)
Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.
Zab 37:8 (SUV)
Ukomeshe hasira, uache ghadhabu, Usikasirike, mwisho wake ni kutenda mabaya.
Mit 14:29 (SUV)
Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi; Bali mwenye roho ya hamaki hutukuza upumbavu.
Mit 15:1 (SUV)
Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.
Mhu 7:9 (SUV)
Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.
Mit 29:11 (SUV)
Mpumbavu hudhihirisha hasira yake yote; Bali mwenye hekima huizuia na kuituliza.
Mit 16:32 (SUV)
Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa; Na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji.
Mit 15:18 (SUV)
Mtu wa hasira huchochea ugomvi; Bali asiye mwepesi wa hasira hutuliza mashindano.
Rum 12:19 (SUV)
Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.
Kol 3:8 (SUV)
Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu.
Zab 76:10 (SUV)
Maana hasira ya binadamu itakusifu, Masalio ya hasira utajifunga kama mshipi.
Zab 2:12 (SUV)
Shikeni yaliyo bora , asije akafanya hasira Nanyi mkapotea njiani, Kwa kuwa hasira yake itawaka upesi; Heri wote wanaomkimbilia.
Zab 95:11 (SUV)
Nikaapa kwa hasira yangu Wasiingie rahani mwangu.
Ebr 3:11 (SUV)
Kama nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia rahani mwangu.
Zab 103:9 (SUV)
Yeye hatateta sikuzote, Wala hatashika hasira yake milele.
Sef 2:2 (SUV)
kabla haijazaa hiyo amri, kabla haijapita siku ile kama makapi, kabla haijawajilia hasira kali ya BWANA, kabla haijawajilia siku ya hasira ya BWANA.
Zab 77:9 (SUV)
Mungu amesahau fadhili zake? Amezuia kwa hasira rehema zake?
Hes 12:9 (SUV)
Hasira za BWANA zikawaka juu yao; naye akaenda zake.
Ayu 9:5 (SUV)
Aiondoaye milima, nayo haina habari, Akiipindua katika hasira zake.
Ayu 5:2 (SUV)
Kwani hasira humwua mtu mpumbavu, Nao wivu humwua mjinga.