Yohane 2

2
Harusi mjini Kana
1Siku ya tatu kulikuwa na harusi mjini Kana,#2:1 Kana: Mji mdogo yapata kilomita 6 kaskazini mwa Nazareti (2:11; 4:46; 21:2). mkoani Galilaya. Mama yake#2:1 Mama yake: Yaani Maria. Mama yake Yesu anatajwa mara kadhaa katika Injili hii ingawa jina lake “Maria” halitajwi (2:12; 6:42; 19:25). Yesu alikuwapo, 2naye Yesu alikuwa amealikwa harusini pamoja na wanafunzi wake. 3Divai ilipokwisha, mama yake akamwambia, “Hawana divai!” 4Yesu akamjibu, “Mama,#2:4 Mama: Kigiriki ni “gune” na maana yake ya kawaida ni “mwanamke”. Katika Kiswahili fasaha kutafsiri hapa kwa neno “mwanamke” kungekuwa na picha nyingine ambayo haikuwako pale awali. usiniambie la kufanya. Saa yangu#2:4 Saa yangu: Katika Yohane ni saa au wakati ambapo hali halisi ya Yesu na nafsi yake vitakapodhihirishwa, na wakati atakapokamilisha kile alichokijia hapa duniani (rejea 7:6,8,30; 8:20). Saa hiyo aghalabu ilifikiwa katika lile juma la mwisho la huduma yake (12:23; 13:1). Usiku ule kabla ya kukamatwa kwake Yesu anasali: “Baba ile saa imefika” (17:1). bado.” 5Hapo mama yake akawaambia watumishi, “Lolote atakalowaambieni, fanyeni.”
6Hapo palikuwa na mitungi sita ya mawe, ambayo kila mmoja uliweza kuchukua kiasi cha madebe mawili au matatu. Ilikuwa imewekwa hapo kufuatana na desturi ya Kiyahudi ya kutawadha.#2:6 Kutawadha: Kuosha aghalabu mikono, miguu na uso kwa ajili ya kuwa safi ili kufanya mambo ya ibada. Kulingana na desturi ya Wayahudi mtu akigusa kitu kilicho najisi kabla ya kula, chochote anachogusa baadaye nacho huwa najisi. 7Yesu akawaambia, “Ijazeni mitungi hiyo maji.” Nao wakaijaza mpaka juu. 8Kisha akawaambia, “Sasa choteni mkampelekee mkuu wa karamu.” 9Mkuu wa karamu alipoonja hayo maji, kumbe yalikuwa yamegeuka kuwa divai. Yeye hakujua ilikotoka, (lakini wale watumishi waliochota maji walijua). Mkuu wa karamu akamwita bwana arusi, 10akamwambia, “Kila mtu huandaa divai nzuri kwanza hata wakisha tosheka huandaa ile hafifu. Lakini wewe umeiweka divai nzuri mpaka sasa!”
11Yesu alifanya ishara#2:11 Ishara: Yohane anatumia neno “ishara” kutaja miujiza ya Yesu na hivyo anaifafanua kuwa vitu vinavyoashiria Yesu ni nani: Mwana wa Mungu. hii ya kwanza huko Kana, Galilaya, akaonesha utukufu wake; nao wanafunzi wake wakamwamini.
12Baada ya hayo, Yesu alishuka pamoja na mama yake, ndugu zake na wanafunzi wake, wakaenda Kafarnaumu#2:12 Kafarnaumu: Mji upande wa kaskazini-magharibi mwa Ziwa Galilaya. ambako walikaa kwa siku chache.
Yesu hekaluni
(Mat 21:12-13; Marko 11:15-17; Luka 19:45-46)
13Sikukuu ya Wayahudi ya Pasaka#2:13 Sikukuu ya …Pasaka: Hii iliadhimishwa kuwakumbusha watu wa Israeli jinsi Mungu alivyowaotoa wazee wao utumwani kule Misri (Kut 12—13). Sikukuu hiyo iliadhimishwa tarehe ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza uitwao Nisani (Machi - Aprili katika kalenda yetu). Mara baada ya sikukuu hiyo, ilianza sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu ambayo ilidumu kwa siku saba. Hii ni sikukuu ya kwanza ya Pasaka kutajwa. Yohane anazo tatu: 6:4; 11:55 na hii ya 2:13. ilikuwa imekaribia; hivyo Yesu akaenda juu Yerusalemu. 14Basi, akawakuta mle hekaluni watu wakiuza ng'ombe, kondoo na njiwa, na wavunja fedha#2:14 Akawakuta hekaluni watu wakiuza ng'ombe, kondoo …na wavunja fedha: Katika ukumbi mmojawapo wa hekalu (ukumbi uliojulikana kama wa watu wa mataifa) makuhani walijipatia fedha nyingi kwa kuuza wanayama wa kutambikia kama ilivyotakiwa na sheria ya Mose. Nao wavunja fedha walibadilisha fedha za kigeni kwa zile sarafu zilizotakiwa kulipa kodi ya mwaka ya hekalu. walikuwa wamekaa kwenye meza zao. 15Akatengeneza mjeledi wa kamba, akawafukuza wote nje ya hekalu pamoja na kondoo na ng'ombe wao, akazitawanya sarafu za wenye kuvunja fedha na kupindua meza zao. 16Akawaambia wale waliokuwa wanauza njiwa, “Ondoeni vitu hivi hapa. Msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa soko!” 17Wanafunzi wake wakakumbuka kwamba Maandiko yasema: “Upendo wangu kwa nyumba yako waniua.”
18Baadhi ya Wayahudi wakamwuliza Yesu, “Utafanya mwujiza gani kuonesha kwamba unayo haki kufanya mambo haya?” 19Yesu akawaambia, “Vunjeni hekalu hili, nami nitalijenga kwa siku tatu.”#2:19 Vunjeni hekalu hili …nitalijenga kwa siku tatu: Taz shtaka walilomtolea wakati wa hukumu yake: Mat 26:60-61; Marko 14:57-59. Maneno ya Yesu yanaweza kuwa na maana ya hilo hekalu na pia ufufuo wake kutoka kwa wafu. 20Hapo Wayahudi wakasema, “Hekalu hili lilijengwa kwa muda wa miaka arubaini na sita. Je, wewe utalijenga kwa siku tatu?”
21Lakini Yesu alikuwa anaongea juu ya hekalu ambalo ni mwili wake. 22Basi, alipofufuliwa kutoka kwa wafu, wanafunzi wake walikumbuka kwamba alikuwa amesema hayo, wakayaamini Maandiko Matakatifu na yale maneno ambayo Yesu alikuwa amesema.
Yesu ajua mioyo ya watu wote
23Yesu alipokuwa Yerusalemu kwa sikukuu ya Pasaka, watu wengi walimwamini walipoona ishara alizofanya. 24Lakini Yesu hakuwa na imani nao kwa sababu aliwajua wote. 25Hakuhitaji kuambiwa chochote juu ya watu, maana aliyajua barabara mambo yote yaliyomo mioyoni mwao.

ที่ได้เลือกล่าสุด:

Yohane 2: BHNTLK

เน้นข้อความ

แบ่งปัน

คัดลอก

None

ต้องการเน้นข้อความที่บันทึกไว้ตลอดทั้งอุปกรณ์ของคุณหรือไม่? ลงทะเบียน หรือลงชื่อเข้าใช้