Luka 20
20
Suala juu ya mamlaka ya Yesu
(Mat 21:23-27; Marko 11:27-33)
1Siku moja, Yesu alipokuwa akiwafundisha watu hekaluni na kuwahubiria juu ya Habari Njema, makuhani wakuu na waalimu wa sheria pamoja na wazee walifika,#20:1-2 Wakuu wa kidini wanamhoji Yesu juu ya matendo yake ambayo yanasimuliwa katika sehemu zilizotangulia (Luka 19:28-48). Mambo haya hapa ni hasa juu ya kule kuwafukuza nje wafanyabiashara hekaluni (19:45). 2wakasema, “Tuambie! Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani?” 3Yesu akawaambia, “Na mimi nitawaulizeni swali: 4mamlaka ya Yohane#20:4 Yohane: Yaani Yohane Mbatizaji Luka 3:1-18; Yoh 1:6-28. ya kubatiza yalitoka kwa Mungu au kwa watu?” 5Lakini wao wakajadiliana hivi: “Tukisema yalitoka kwa Mungu, yeye atatuuliza: ‘Mbona hamkumsadiki?’ 6Na tukisema yalitoka kwa binadamu, watu wote hapa watatupiga mawe, maana wote wanaamini kwamba Yohane alikuwa nabii.” 7Basi, wakamwambia, “Hatujui mamlaka hayo yalitoka wapi.” 8Yesu akawaambia, “Hata mimi sitawaambia ninafanya mambo haya kwa mamlaka gani.”
Mfano wa shamba la mizabibu na wakulima
(Mat 21:33-46; Marko 12:1-12)
9Yesu akaendelea kuwaambia watu mfano huu: “Mtu mmoja alilima shamba la mizabibu,#20:9 Shamba la mizabibu: Mfano wa Israeli pamoja na dokezo juu ya Isa 5:1-7; taz Mat 21:33 ambapo yadhihirika kwamba ilikuwa kawaida kufananisha Israeli na shamba la mizabibu. akalikodisha kwa wakulima; kisha akasafiri hadi nchi ya mbali, akakaa huko kwa muda mrefu.#20:9 Kwa kutumia lugha ya A.K. (taz Isa 5:1-7) Yesu anatoa simulizi ambalo wasikilizaji wake walilielewa vizuri sana: Viongozi wa dini hawakushika maagano Mungu aliyofanya nao; waliwakataa wajumbe wake na hata kumwua mwana wa huyo mwenye shamba yaani Mwana wa Mungu. Matokeo yake ni aya 16: Atawapa wengine shamba hilo yaani, Mungu atawapa wengine jukumu la kuwatunza watu wake. 10Wakati wa mavuno, mtu huyo alimtuma mtumishi wake kwa wale wakulima, akachukue sehemu ya matunda ya shamba la mizabibu. Lakini wale wakulima wakampiga mtumishi huyo, wakamrudisha mikono mitupu. 11Yule bwana akamtuma tena mtumishi mwingine; lakini wao wakampiga huyo vilevile na kumtendea vibaya, wakamrudisha mikono mitupu. 12Akamtuma tena wa tatu; huyu naye, baada ya kumwumiza, wakamfukuza. 13Yule mwenye shamba akafikiri: ‘Nitafanya nini? Nitamtuma mwanangu mpenzi;#20:13 Mwanangu mpenzi: Yawezekana kueleweka pia kama Mwanangu wa pekee. Hapa tunakumbushwa maneno yaleyale yaliyotumiwa wakati wa ubatizo wa Yesu (3:27) na kugeuka sura kwa Yesu (9:35). labda watamjali yeye.’ 14Wale wakulima walipomwona tu, wakasemezana: ‘Huyu ndiye mrithi.#20:14 Mrithi: Kwa kusema hivyo hapa yadokezwa kwamba huyo mwenye shamba alikuwa na mtoto mmoja tu. Basi, tumuue ili urithi wake uwe wetu.’ 15Basi, wakamtoa nje ya lile shamba la mizabibu, wakamuua.” Yesu akauliza, “Yule mwenye shamba atawafanya nini hao wakulima? 16Atakuja kuwaangamiza wakulima hao, na kuwapa wakulima wengine hilo shamba la mizabibu.” Watu waliposikia maneno hayo, walisema: “Hasha! Yasitukie hata kidogo!”
17Lakini Yesu akawatazama, akawaambia, “Maandiko haya Matakatifu yana maana gani, basi?
‘Jiwe walilokataa waashi,
sasa limekuwa jiwe kuu la msingi!’#20:17 Jiwe kuu la msingi: Zab 118:22. Zaburi hiyo inakaririwa kumhusu Yesu mwenyewe ambaye alikataliwa na kudharauliwa na viongozi wa kidini wa Waisraeli, lakini yeye amekuwa na amedhihirika kwamba ndiye ambaye kwa njia yake Mungu amejionesha miongoni mwa watu wake (Taz Marko 12:10-11; Rom 9:31-33; 1Pet 2:6-8).
18Mtu yeyote akianguka juu ya jiwe hilo atavunjika vipandevipande; na likimwangukia mtu yeyote, litamponda.”
Kulipa kodi kwa Kaisari
(Mat 22:15-22; Marko 12:13-17)
19Waalimu wa sheria na makuhani wakuu walifahamu kwamba mfano huo ulikuwa unawahusu, na hivyo walitaka kumkamata palepale, ila tu waliogopa watu. 20Basi, wakawa wanatafuta wakati wa kufaa. Wakawahonga watu fulani wajisingizie kuwa wema, wakawatuma wamnase Yesu kwa maswali, na hivyo waweze kumtia nguvuni na kumpeleka kwa wakuu wa serikali. 21Hao wapelelezi wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba unasema na kufundisha mambo ya kweli; tunajua kwamba wewe huna ubaguzi; wewe wafundisha ukweli juu ya njia ya Mungu. 22Basi, tuambie kama ni halali au la, kulipa kodi kwa Kaisari!”#20:22 Kuhusu swali hilo taz Mat 22:17.
23Yesu alitambua mtego wao, akawaambia, 24“Nionesheni sarafu.#20:24-25 Sarafu: Sarafu ya fedha ya Kiroma ambayo wakati huo ilikuwa na chapa ya Kaisari Tiberio, mtawala mkuu wa Roma, na maneno “Tiberio Kaisari, mwana wa mungu Augusto” kuizunguka. Je, sura na chapa ni vya nani?” 25Nao wakamjibu, “Ni ya Kaisari.” Yesu akawaambia, “Basi, ya Kaisari mpeni Kaisari, na ya Mungu mpeni Mungu.” 26Hawakufaulu kumnasa kwa neno lolote pale mbele ya watu na hivyo wakakaa kimya wakilistaajabia jibu lake.
Suala juu ya ufufuo
(Mat 22:23-33; Marko 12:18-27)
27Kisha Masadukayo, ambao husema kwamba wafu hawafufuki, wakamjia Yesu, wakasema:#20:27 Ling Mate 4:1-2; 23:8. Masadukayo walikuwa wanachama wa kikundi cha kidini cha Wayahudi ambacho kilitofautiana na kikundi cha Mafarisayo kwa vile hawa waliamini kuweko kwa ufufuo wa wafu hali Masadukayo hawakuamini hayo. Masadukayo walithamini vitabu vitano vya kwanza vya Biblia kuwa ndivyo vitabu vitakatifu peke yake. Jibu la Yesu lina sehemu mbili: (a) Nyakati zijazo, watu waliofufuka katika wafu hawatakufa tena na hivyo, kama vile malaika, hawatahitaji kuoa (aya 35-36); (b) Yesu anakariri Kut 3:6 kama hakikisho kwamba Abrahamu, Isaka na Yakobo wanaishi, maana Mungu anatajwa kuwa Mungu wao, kitu ambacho hakingewezekana kama hawakuwa hai. 28“Mwalimu, Mose alituandikia kwamba kama ndugu ya mtu fulani akifa na kumwacha mjane wake bila watoto, ni lazima ndugu yake amchukue huyo mama mjane, ili ampatie ndugu yake watoto. 29Sasa, wakati mmoja kulikuwa na ndugu saba. Yule wa kwanza alioa na baadaye akafa bila kuacha mtoto. 30Yule ndugu wa pili akamwoa yule mjane, naye pia akafa; 31na ndugu wa tatu vilevile. Mambo yakawa yaleyale kwa wote saba — wote walikufa bila kuacha watoto. 32Mwishowe akafa pia yule mwanamke. 33Je, siku wafu watakapofufuliwa, mama huyo atakuwa mke wa nani? Maana wote saba walikuwa wamemwoa.”
34Yesu akawaambia, “Watu wa nyakati hizi huoa na kuolewa; 35lakini wale ambao Mungu atawawezesha kushiriki ule wakati wa ufufuo, hawataoa wala kuolewa. 36Ama hakika, hawawezi kufa tena, kwa sababu watakuwa kama malaika, na ni watoto wa Mungu kwa vile wamefufuliwa katika wafu. 37Lakini, kwamba kuna kufufuka kutoka kwa wafu, hata Mose alithibitisha jambo hilo katika Maandiko Matakatifu. Katika sehemu ya Maandiko Matakatifu juu ya kile kichaka kilichokuwa kinawaka moto, anamtaja Bwana kama Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo.#20:37-38 Yesu anagusia Kut 3:2-6. Mungu … wa walio hai: Yaani Abrahamu na Isaka na Yakobo ambao walikufa, wako hai. 38Basi, yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa wale walio hai; maana kwake wote wanaishi.”
39Baadhi ya wale waalimu wa sheria wakasema, “Mwalimu, umejibu vema kabisa.” 40Walisema hivyo kwa sababu hawakuthubutu kumwuliza tena maswali mengine.
Suala juu ya Kristo
(Mat 22:41-46; Marko 12:35-37)
41Yesu akawauliza, “Yasemekanaje kwamba Kristo ni mwana wa Daudi?#20:41 Watu walitumaini kwamba Masiha angekuwa mzaliwa wa ukoo wa mfalme Daudi. 42Daudi mwenyewe anasema katika Zaburi:
‘Bwana alimwambia Bwana wangu:
Keti upande wangu wa kulia#20:42 Upande wangu wa kulia: Mahali pa heshima.
43mpaka niwaweke maadui zako kuwa kiti cha kuwekea miguu yako.’#20:42-43 Maadui zako kuwa kiti cha kuwekea miguu yako: Zab 110:1. Kuwafanya maadui hivyo maana yake ni kuwashinda kabisa na kuwaangamiza.
44Ikiwa Daudi anamwita yeye, ‘Bwana,’ basi, atakuwaje mwanawe?”
Yesu anawaonya watu kuhusu waalimu wa sheria
(Mat 23:1-36; Marko 12:38-40)
45Yesu aliwaambia wanafunzi wake mbele ya watu wote, 46“Jihadharini na waalimu wa sheria ambao hupenda kupitapita wamevalia kanzu. Hupenda kusalimiwa na watu kwa heshima masokoni, huketi mahali pa heshima katika masunagogi na kuchukua nafasi za heshima katika karamu. 47Huwadhulumu wajane huku wakisingizia kuwa wema kwa kusali sala ndefu. Hao watapata hukumu kali zaidi!”
ที่ได้เลือกล่าสุด:
Luka 20: BHNTLK
เน้นข้อความ
แบ่งปัน
คัดลอก
ต้องการเน้นข้อความที่บันทึกไว้ตลอดทั้งอุปกรณ์ของคุณหรือไม่? ลงทะเบียน หรือลงชื่อเข้าใช้
Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993
The Bible Society of Kenya 1993

: