Luka 21
21
Sadaka ya mama mjane
(Marko 12:41-44)
1Yesu alitazama kwa makini, akawaona matajiri walivyokuwa wanatia sadaka zao katika hazina ya hekalu, 2akamwona pia mama mmoja mjane akitumbukiza humo sarafu mbili ndogo. 3Basi, akasema, “Nawaambieni kweli, mama huyu mjane maskini ametia katika hazina kiasi kikubwa kuliko walichotia wote. 4Kwa maana, wengine wote wametoa sadaka zao kutokana na ziada ya mali zao, lakini huyu mama, ingawa ni maskini, ametoa kila kitu alichohitaji kwa kuishi.”
Yesu anatabiri kuharibiwa kwa hekalu
(Mat 24:1-2; Marko 13:1-2)
5Baadhi ya wanafunzi walikuwa wanazungumza juu ya hekalu, jinsi lilivyopambwa kwa mawe ya thamani, pamoja na sadaka zilizotolewa kwa Mungu. Yesu akasema,#21:5 Sehemu ya mbele ya ukuta wa hekalu ilikuwa ya marumaru, imepambwa kwa vito vya thamani ambavyo watu walimtolea Mungu, mojawapo kikiwa kifuniko kikubwa juu ya lango ambacho kilitolewa na Herode Mkubwa. (Taz maelezo ya Marko 13:1). 6“Haya yote mnayoyaona — zitakuja siku ambapo hakuna hata jiwe moja litakalosalia juu ya lingine; kila kitu kitaharibiwa.”#21:6 Mji wa Yerusalemu uliteketezwa na jeshi la Waroma mwaka wa 70 B.K. Katika sura hii tukio hilo linagusiwa kiasi na pia kwa upande mmoja juu ya kurudi kwake Mwana wa Mtu mwishoni mwa dunia.
Taabu na mateso
(Mat 24:3-14; Marko 13:3-13)
7Basi, wakamwuliza, “Mwalimu, mambo hayo yatatokea lini? Na ni ishara gani zitakazoonesha kwamba karibu mambo hayo yatokee?”
8Yesu akawajibu, “Jihadharini, msije mkadanganyika. Maana wengi watatokea na kulitumia jina langu, kila mmoja akidai kwamba yeye ni mimi, na kwamba wakati ule umekaribia. Lakini nyinyi msiwafuate!#21:8-11 Jibu la Yesu katika aya hizi linasema mambo ambayo yanahusu mengine yasiyo ya hekalu ambalo liliharibiwa mwaka wa 70 B.K.: juu ya ishara za mwisho wa nyakati (aya 9). Lugha ya aya ya 11 inafanana na lugha ya Isa 8:21-22; Eze 5:11-12. 9Basi, mtakaposikia habari za vita na misukosuko, msitishike; maana ni lazima hayo yatokee kwanza, lakini mwisho wa yote, bado.”
10Halafu akaendelea kusema: “Taifa moja litapigana na taifa lingine, na ufalme mmoja utapigana na ufalme mwingine. 11Kila mahali kutakuwa na mitetemeko mikubwa ya ardhi, njaa na tauni. Kutakuwa na vituko vya kutisha na ishara kubwa angani. 12Lakini kabla ya kutokea hayo yote, watawatieni nguvuni, watawatesa na kuwapelekeni katika masunagogi na kuwatia gerezani; mtapelekwa mbele ya wafalme na watawala kwa ajili ya jina langu, 13mpate kunishuhudia kwao. 14Muwe na msimamo huu mioyoni mwenu: hakuna kufikiria kabla ya wakati juu ya jinsi mtakavyojitetea, 15kwa sababu mimi mwenyewe nitawapeni ufasaha wa maneno na hekima, hata maadui zenu hawataweza kustahimili wala kupinga. 16Wazazi wenu, ndugu, jamaa na rafiki zenu watawasaliti nyinyi; na baadhi yenu mtauawa. 17Watu wote watawachukieni nyinyi kwa sababu ya jina langu. 18Lakini, hata unywele mmoja wa vichwa vyenu hautapotea. 19Kwa uvumilivu wenu, mtayaokoa maisha yenu.
Yesu anatabiri kuharibiwa kwa mji wa Yerusalemu
(Mat 24:15-21; Marko 13:14-19)
20“Mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, basi jueni ya kwamba wakati umefika ambapo mji huo utaharibiwa. 21Hapo, walioko Yudea wakimbilie milimani; wale walio mjini watoke; na wale walio mashambani wasirudi mjini. 22Kwa maana siku hizo ni siku za adhabu, ili yote yaliyoandikwa yatimie. 23Ole wao waja wazito na wanyonyeshao siku hizo! Kwa maana kutakuwa na dhiki kubwa katika nchi, na hasira ya Mungu itawajia watu hawa. 24Wengine watauawa kwa upanga, wengine watachukuliwa mateka katika nchi zote; na mji wa Yerusalemu utakanyagwa na watu wa mataifa mengine, hadi nyakati zao zitakapotimia.
Kuja kwake Mwana wa Mtu
(Mat 24:29-31; Marko 13:24-27)
25“Kutakuwa na ishara katika jua na mwezi na nyota. Mataifa duniani yatakuwa na dhiki kwa sababu ya wasiwasi kutokana na mshindo wa mawimbi ya bahari. 26Watu watazirai kwa sababu ya woga, wakitazamia mambo yatakayoupata ulimwengu; kwa maana nguvu za mbingu#21:26 Nguvu za mbingu: Nyota na sayari ambazo zilifikiriwa kuwa chini ya uongozi na mamlaka ya nguvu za kiroho. zitatikiswa. 27Halafu, watamwona Mwana wa Mtu akija katika wingu, mwenye nguvu na utukufu mwingi. 28Wakati mambo hayo yatakapoanza kutukia, simameni na kuinua vichwa vyenu juu, kwa maana ukombozi wenu umekaribia.”
Mfano wa mtini
(Mat 24:32-35; Marko 13:28-31)
29Kisha akawaambia mfano: “Angalieni mtini na miti mingine yote. 30Mnapoona kwamba imeanza kuchipua majani, mwatambua kwamba majira ya mavuno yamekaribia. 31Vivyo hivyo, mtakapoona mambo hayo yanatendeka, mtatambua kwamba ufalme wa Mungu umekaribia. 32Kweli nawaambieni, kizazi hiki cha sasa hakitapita kabla ya hayo yote kutendeka. 33Mbingu na dunia zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Lazima kuwa macho
34“Muwe macho, mioyo yenu isije ikalemewa na anasa, ulevi na shughuli za maisha haya. La sivyo, siku ile itawajieni ghafla. 35Kwa maana itawajia kama mtego wote wanaoishi duniani pote. 36Muwe waangalifu basi, na salini daima#21:36 Salini daima: Taz maelezo ya Luka 18:1 ili muweze kupata nguvu ya kupita salama katika mambo haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele ya Mwana wa Mtu.”
37Wakati wa mchana, siku hizo, Yesu alikuwa akifundisha watu hekaluni; lakini usiku alikuwa akienda katika mlima wa Mizeituni na kukaa huko. 38Watu wote walikuwa wanakwenda hekaluni asubuhi na mapema, wapate kumsikiliza.
ที่ได้เลือกล่าสุด:
Luka 21: BHNTLK
เน้นข้อความ
แบ่งปัน
คัดลอก
ต้องการเน้นข้อความที่บันทึกไว้ตลอดทั้งอุปกรณ์ของคุณหรือไม่? ลงทะเบียน หรือลงชื่อเข้าใช้
Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993
The Bible Society of Kenya 1993

: