Mwanzo 6

6
Gharika kuu
1Idadi ya watu ilipoanza kuongezeka duniani, na watoto wa kike wakazaliwa kwao, 2wana wa Mungu wakawaona kuwa hao binti za wanadamu walikuwa wazuri wa sura, wakaoa yeyote miongoni mwao waliyemchagua. 3Ndipo Mwenyezi Mungu akasema, “Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye ni wa kufa; siku zake zitakuwa miaka mia moja na ishirini.”
4Wanefili walikuwa duniani siku hizo, na hata baadaye, hao wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu na kuzaa nao. Wanefili walikuwa mashujaa wa zamani, na watu mashuhuri.
5Mwenyezi Mungu akaona jinsi uovu wa mwanadamu ulivyokuwa mkubwa duniani, na ya kuwa kila mwelekeo wa mawazo ya moyo wake wakati wote ulikuwa mbaya tu. 6Mwenyezi Mungu akasikitika kwamba alimuumba mwanadamu duniani, na moyo wa Mungu ukasikitika sana. 7Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akasema, “Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemuumba kutoka uso wa dunia, wanadamu na wanyama, pamoja na viumbe vinavyotambaa ardhini, na ndege wa angani. Kwa maana nasikitika kuwaumba.” 8Lakini Nuhu akapata kibali machoni pa Mwenyezi Mungu.
9Hivi ndivyo vizazi vya Nuhu.
Nuhu alikuwa mtu wa haki, na mkamilifu miongoni mwa watu wa wakati wake, tena alitembea na Mungu. 10Nuhu alikuwa na wana watatu: Shemu, Hamu na Yafethi.
11Wakati huu dunia ilikuwa imejaa uharibifu na ukatili machoni pa Mungu. 12Mungu akaona jinsi dunia ilivyoharibika, kwa maana watu wote duniani walikuwa wameharibu njia zao. 13Kwa hiyo Mungu akamwambia Nuhu, “Nitawaangamiza watu wote, kwa kuwa dunia imejaa ukatili kwa sababu yao. Hakika nitaangamiza watu pamoja na dunia. 14Kwa hiyo jitengenezee safina kubwa kwa mbao za mvinje; tengeneza vyumba ndani yake na uipake lami ndani na nje. 15Hivi ndivyo utakavyoitengeneza: Safina iwe na urefu wa dhiraa mia tatu#6:15 Dhiraa 300 ni sawa na mita 135., upana wake dhiraa hamsini#6:15 Dhiraa 50 ni sawa na mita 22:5., na kimo chake dhiraa thelathini#6:15 Dhiraa 30 ni sawa na mita 13:5.. 16Itengenezee paa na umalizie safina kwa kuacha nafasi ya dhiraa moja#6:16 Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45. juu. Weka mlango ubavuni mwa safina, na uifanye ya ghorofa ya chini, ya kati na ya juu. 17Nitaleta gharika ya maji juu ya dunia ili kuangamiza kila chenye uhai chini ya mbingu, kila kiumbe chenye pumzi ya uhai ndani yake. Kila kitu juu ya dunia kitaangamia. 18Lakini mimi nitaweka agano langu na wewe, nawe utaingia ndani ya Safina, wewe pamoja na mke wako, wanao na wake zao. 19Utaingiza ndani ya Safina kila aina ya kiumbe hai wawili wawili, wa kiume na wa kike, ili kuwahifadhi hai pamoja na wewe. 20Wawili wa kila aina ya ndege, wa kila aina ya mnyama, na wa kila aina ya kiumbe kinachotambaa ardhini watakuja kwako ili wahifadhiwe hai. 21Utachukua kila aina ya chakula kitakacholiwa, na ukiweke akiba kama chakula kwa ajili yako na yao.”
22Nuhu akafanya kila kitu kama vile Mungu alimwamuru.

Currently Selected:

Mwanzo 6: NENO

Qaqambisa

Share

Copy

None

Ufuna ukuba iimbalasane zakho zigcinwe kuzo zonke izixhobo zakho? Bhalisela okanye ngena