Luka 20:46-47

Luka 20:46-47 SWC02

“Mujiepushe na walimu wa Sheria wanaopenda kujitembeza, wakivaa kanzu ndefu na kusalimiwa kwa heshima kwenye nafasi za makutano. Wanapenda vilevile kuikaa katika viti vya mbele ndani ya nyumba za kuabudia, na kwenye nafasi za heshima katika karamu. Wananyanganya mali ya wajane na kuomba maombi marefu kusudi waonekane mbele ya watu. Kwa sababu hii watahukumiwa vikali sana!”