Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu,
Mkombozi wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli:
“Mimi ni Mwenyezi Mungu, Mungu wako,
nikufundishaye ili upate faida,
nikuongozaye katika njia ikupasayo kuiendea.
Laiti ungesikiliza kwa makini maagizo yangu,
amani yako ingekuwa kama mto,
haki yako kama mawimbi ya bahari.