1
Isaya 60:1
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
“Ondoka, angaza, kwa kuwa nuru yako imekuja na utukufu wa Mwenyezi Mungu umezuka juu yako.
Compare
Explore Isaya 60:1
2
Isaya 60:3
Mataifa watakuja kwenye nuru yako na wafalme kwa mwanga wa mapambazuko yako.
Explore Isaya 60:3
3
Isaya 60:2
Tazama, giza litaifunika dunia, na giza nene litayafunika mataifa, lakini Mwenyezi Mungu atazuka juu yako na utukufu wake utaonekana juu yako.
Explore Isaya 60:2
4
Isaya 60:22
Aliye mdogo kwenu atakuwa elfu, mdogo kuliko wote atakuwa taifa lenye nguvu. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu; katika wakati wake nitayatimiza haya upesi.”
Explore Isaya 60:22
5
Isaya 60:19
Jua halitakuwa tena nuru yako mchana, wala mwangaza wa mwezi hautakuangazia, kwa maana Mwenyezi Mungu atakuwa nuru yako ya milele, naye Mungu wako atakuwa utukufu wako.
Explore Isaya 60:19
6
Isaya 60:20
Jua lako halitazama tena, nao mwezi wako hautafifia tena; Mwenyezi Mungu atakuwa nuru yako milele, nazo siku zako za huzuni zitakoma.
Explore Isaya 60:20
7
Isaya 60:5
Ndipo utatazama na kutiwa nuru, moyo wako utasisimka na kujaa furaha, mali iliyo baharini italetwa kwako, utajiri wa mataifa utakujilia.
Explore Isaya 60:5
8
Isaya 60:4
“Inua macho yako na utazame pande zote: Wote wanakusanyika na kukujia, wana wako wanakuja toka mbali, nao binti zako wanabebwa mikononi.
Explore Isaya 60:4
9
Isaya 60:21
Ndipo watu wako wote watakuwa waadilifu, nao wataimiliki nchi milele. Wao ni chipukizi nililolipanda, kazi ya mikono yangu, ili kuonesha utukufu wangu.
Explore Isaya 60:21
10
Isaya 60:18
Jeuri hazitasikika tena katika nchi yako, wala maangamizi au uharibifu ndani ya mipaka yako, lakini utaita kuta zako Wokovu, na malango yako Sifa.
Explore Isaya 60:18
11
Isaya 60:11
Malango yako yatakuwa wazi siku zote, kamwe hayatafungwa, mchana wala usiku, ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa: wafalme wao wakiongoza maandamano ya ushindi.
Explore Isaya 60:11
12
Isaya 60:6
Makundi ya ngamia yatajaa katika nchi yako, ngamia vijana wa Midiani na Efa. Nao watu wote wanaotoka Sheba watakuja, wakichukua dhahabu na uvumba na kutangaza sifa za Mwenyezi Mungu.
Explore Isaya 60:6
13
Isaya 60:10
“Wageni watazijenga upya kuta zako, na wafalme wao watakutumikia. Ingawa katika hasira nilikupiga, lakini katika upendeleo wangu nitakuonesha huruma.
Explore Isaya 60:10
14
Isaya 60:15
“Ingawa umeachwa na kuchukiwa, bila yeyote anayesafiri ndani yako, nitakufanya kuwa fahari ya milele, na furaha ya vizazi vyote.
Explore Isaya 60:15
15
Isaya 60:16
Utanyonya maziwa ya mataifa, na kunyonyeshwa matiti ya wafalme. Ndipo utakapojua kwamba Mimi, Mwenyezi Mungu, ni Mwokozi wako, Mkombozi wako, niliye Mwenye Nguvu wa Yakobo.
Explore Isaya 60:16
Home
Bible
Plans
Videos