YouVersion Logo
Search Icon

Tito Utangulizi

Utangulizi
Tito, kama vile Timotheo, alikuwa mshirika na rafiki wa karibu wa Paulo katika huduma yake. Alikuwa muumini asiyetahiriwa, mtu wa Mataifa kutoka Antiokia. Alifuatana na Paulo na Barnaba kuhudhuria Baraza la Yerusalemu. Paulo alimwandikia Tito waraka huu muda mfupi tu baada ya kumwachia wajibu wa kuliangalia na kuliimarisha kundi la waumini la Krete. Tito alikuwa na wajibu wa kuwateua wazee wa kundi la waumini, kuwaweka wakfu, na kuwafundisha kushika misingi ya imani ya wafuasi wa Al-Masihi.
Waraka huu unaonesha kuwa kundi la waumini la Krete halikuwa na mpangilio mahsusi. Ilimbidi Paulo aeleze kwa kina kuhusu sifa za wazee wa kundi la waumini, na pia kutoa mafundisho kwa waumini. Paulo aligusia matatizo yanayowapata watumishi wa Mwenyezi Mungu, na jinsi yanavyoweza kutatuliwa.
Mwandishi
Mtume Paulo.
Kusudi
Kumshauri Tito kuhusu wajibu wake wa uangalizi wa makundi ya waumini katika kisiwa cha Krete.
Mahali
Pengine ni Korintho.
Tarehe
Mnamo 64 B.K.
Wahusika Wakuu
Paulo na Tito.
Wazo Kuu
Ingawa katika maisha yetu hapa duniani tumezungukwa na uovu na chuki, hatuna budi maisha yetu kuwa kielelezo jinsi neema ya Mwenyezi Mungu inatupatia ushindi.
Mambo Muhimu
Kuweka mpango na uangalizi wa makundi ya waumini, na jinsi ya kufanya kazi hiyo. Mkazo wa barua hii ni kuhusu kuishi maisha matakatifu katika Al-Masihi katikati ya uovu ulioko duniani. Paulo anarudia mara kwa mara kusisitiza kudumisha matendo mema.
Yaliyomo
Salamu, na wajibu wa Tito huko Krete (1:1-16)
Fundisha wote mafundisho manyofu (2:1-15)
Maagizo mbalimbali, na maneno ya mwisho (3:1-15).

Currently Selected:

Tito Utangulizi: NENO

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in