YouVersion Logo
Search Icon

Mit 13

13
1 # 1 Sam 2:25; Mit 9:7,8 Mwana mwenye hekima husikiliza mausia ya babaye;
Bali mwenye dharau hasikilizi maonyo.
2Mtu atakula mema kwa matunda ya kinywa chake;
Bali nafsi ya mtu haini itakula jeuri.
3 # Zab 39:1 Yeye alindaye kinywa chake huilinda nafsi yake;
Bali afunuaye midomo yake atapata uharibifu.
4Nafsi ya mtu mvivu hutamani asipate kitu;
Bali nafsi ya mwenye bidii itanenepeshwa.
5 # Kol 3:9; Rum 12:9 Mwenye haki huchukia kusema uongo;
Bali mtu mbaya huwa karaha, hupatwa na aibu.
6 # Mit 11:3 Haki humlinda yeye aliye mnyofu katika njia yake;
Bali ubaya humwangusha mwenye dhambi.
7Kuna mtu mwenye kujitajirisha, lakini hana kitu;
Kuna ajifanyaye kuwa maskini, lakini ana mali nyingi.
8Dia ya nafsi ya mtu ni utajiri wake;
Bali mtu maskini hasikii ogofyo lo lote.
9Nuru ya mwenye haki yang’aa sana;
Bali taa ya mtu mbaya itazimika.
10Kiburi huleta mashindano tu;
Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana.
11 # Mit 20:21 Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka;
Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa.
12Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua.
Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima.
13 # 2 Nya 36:16 Kila alidharauye neno hujiletea uharibifu;
Bali yeye aiogopaye amri atapewa thawabu.
14 # Mit 16:22; 15:24; 2 Sam 22:6; Zab 116:3 Sheria ya mwenye akili ni chemchemi ya uzima,
Ili kuepukana na tanzi za mauti.
15Ufahamu mwema huleta upendeleo;
Bali njia ya haini huparuza.
16 # Mit 12:23 Kila aliye na busara hutenda kazi kwa maarifa;
Bali mpumbavu hueneza upumbavu.
17Mjumbe mbaya huanguka maovuni;
Bali mjumbe mwaminifu ni afya.
18 # Mit 15:5 Umaskini na fedheha zitampata yeye akataaye kurudiwa;
Bali yeye aangaliaye maonyo ataheshimiwa.
19Haja iliyopatikana ni tamu nafsini mwa mtu;
Bali kujitenga na maovu ni chukizo kwa wapumbavu.
20Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima;
Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.
21 # Zab 32:10 Uovu huwaandamia wenye dhambi;
Bali mwenye haki atalipwa mema.
22 # Mhu 2:26 Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi;
Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.
23 # Mit 12:11 Chakula kingi chapatikana kwa ukulima wa maskini;
Bali viko viharibiwavyo kwa sababu ya dhuluma.
24 # Mit 19:18; 22:15 Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe;
Bali yeye ampendaye humrudi mapema.
25Mwenye haki hula akaishibisha nafsi yake;
Bali tumbo la mtu mbaya litaona njaa.

Currently Selected:

Mit 13: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in