Yohana MT. 10
10
1AMIN, amin, nawaambieni, asiyeingia kwa mlango katika zizi la kondoo, lakini apanda penginepo, huyu ni mwizi na mnyangʼanyi. 2Aingiae kwa mlango ni mchunga wa kondoo. 3Bawabu humfungulia huyu, na kondoo humsikia sauti yake, nae huwaita kondoo zake kwa majina yao, huwapeleka nje. 4Awatoapo nje kondoo zilizo zake, huwatangulia; na kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake. 5Mgeni hawatamfuata kabisa, hali watamkimbia, kwa maana hawaijui sauti ya wageni. 6Methali hii Yesu aliwaambia; lakini wao hawakuelewa na mambo hayo aliyowaambia. 7Bassi Yesu aliwaamhia tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi niliye mlango wa kondoo; 8wote walionitangulia ni wezi na wanyangʼanyi: lakini kondoo hawakuwasikia. 9Mimi ndimi niliye mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka, ataingia, atatoka, na atapata malisho. 10Mwizi haji illa aibe, achinje, aharibu; mimi nalikuja wawe na uzima, na wawe nao tele. 11Mimi ndimi niliye mchunga aliye mwema: mchunga aliye mwema huweka maisha yake kwa ajili ya kondoo. 12Mtu wa mshahara, na asiye mchunga, ambae kondoo si mali yake, humwona mbwa wa mwitu anakuja, huziacha kondoo, hukimbia; na mbwa wa mwitu huziteka, huzitawanya. 13Mtu wa mshahara hukimhia kwa kuwa ni mtu wa mshahara, wala hatii moyoni mambo ya kondoo. 14Mimi ndimi niliye mchunga aliye mwema; na walio wangu nawajua, na walio wangu wananijua, 15kama vile Baba anijuavyo, na mimi nimjuavyo Baba: na uzima wangu nauweka kwa ajili ya kondoo. 16Na kondoo wengine ninao, wasio wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta, na sauti yangu wataisikia; na kutakuwapo kundi moja na mchunga mmoja. 17Ndio maana Baba anipenda, kwa sababu nauweka uzima wangu illi niutwae tena. 18Hakuna mtu aniondoleae, bali mimi nauweka mwenyewe. Nina uweza wa kuuweka, tena nina uweza wa kuutwaa tena. Agizo hili nalilipokea kwa Baba yangu.
19Yakaingia tena matangukano katika Wayahudi, kwa ajili ya maneno haya. 20Wengi wao wakasema, Ana pepo, tena ana wazimu; mbona mnamsikiliza? 21Wengine wakasema, Maneno haya siyo ya mtu mwenye pepo. Je! pepo aweza kuwafumbua macho vipofu? 22Bassi ilikuwa siku kuu ya kutabaruku huko Yerusalemi; ni wakati wa baridi. 23Na Yesu alikuwa akitembea ndani ya hekalu, katika ukumbi wa Sulemani. 24Bassi Wayahudi wakamzunguka, wakamwambia, Hatta lini utatuangaisha roho zetu? Kama wewe u Kristo, tuambie wazi wazi. 25Yesu akawajibu, Naliwaambieni, nanyi hamwamini; kazi hizi ninazozifanya kwa jina la Baba yangu, ndizo zinazonishuhudia. 26Lakini ninyi hamwamini kwa sababu hammo katika kondoo zangu, kama nilivyowaambieni. 27Kondoo zangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata; 28nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe, wala hakuna mtu atakaewapokonya katika mkono wangu. 29Baba yangu aliyenipa ni mkuu kuliko wote; wala hakuna awezae kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu. 30Mimi na Baba yangu tu nmoja. 31Bassi Wayahudi wakaokota mawe tena, illi wampige. 32Yesu akawajibu, Kazi njema nyingi nimewaonyesha zitokazo kwa Baba yangu: katika kazi hizo ni ipi mnayonipigia mawe? 33Wayahudi wakamjibu wakinena, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi mawe, bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe, uliye mwana Adamu, wajifanya nafsi yako u Mungu. 34Yesu akawajibu, Haikuandikwa katika torati yenu, ya kama, Mimi nilisema, Ninyi m miungu? 35Ikiwa aliwaita wale miungu waliojiliwa na neno la Mungu (na maandiko hayawezi kutanguka), 36je! yeye ambae Baba alimtakasa akamtuma ulimwenguni, ninyi mwamwambia, Unakufuru, kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu? 37Kama sizitendi kazi za Baba yangu, msiniamini; 38lakini nikizitenda, ijapokuwa hamniamini mimi, ziaminini zile kazi, mpate kujua na kuamini ya kuwa Baba yu ndani yangu, nami ni ndani ya Baba. 39Wakatafuta marra ya pili kumkamata: akatoka mikononi mwao.
40Akaenda zake tena ngʼambu ya Yardani, hatta pahali ptile alipokuwa Yohana akihatiza hapo kwanza; akakaa huko. Watu wengi wakamwendea, wakanena, 41Yohana hakufanya ishara yo yote, lakini yote aliyosema Yohana katika khabari zake huyu yalikuwa kweli. 42Wengi wakamwamini huko.
Currently Selected:
Yohana MT. 10: SWZZB1921
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.