YouVersion Logo
Search Icon

Yohana MT. 11

11
1BASSI mtu mmoja alikuwa hawezi, Lazaro wa Bethania, mtu wa mji wa Mariamu na Martha dada yake. 2Ni Mariamu yule aliyempaka Bwana marhamu, akamfuta miguu yake kwa nywele zake, ambae ndugu yake Lazaro alikuwa hawezi. 3Bassi wale maumbu wakatuma ujumbe kwake, wakisema, Bwana, yeye umpendae hawezi. 4Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali kwa ajili ya utukufu wake Mungu, illi Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo. 5Nae Yesu alimpenda Martha na dada yake ua Lazaro. 6Bassi aliposikia kwamba hawezi alikaa bado siku mbili mahali pale alipokuwapo. 7Kiisha baada ya haya akawaambia wanafunzi wake, Twende Yahudi tena. 8Wale wanafunzi wakamwambia, Rabbi, juzi juzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga mawe, nawe unakweuda huko tena? 9Yesu akajibu, Saa za mchana je si thenashara? Mtu akienda mchana hajikwai, kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu. 10Bali akienda usiku, hujikwaa, kwa sababu nuru haimo ndani yake. 11Aliyasema haya: kiisha baada ya liaya akawaambia, Lazaro rafiki yetu amelala; lakini ninakwenda nipate kumwamsha. 12Bassi wale wanafunzi wake wakamwambia, Bwana, kama amelala atapona. 13Lakini Yesu amenena khabari za mauti yake: nao walidhani ya kuwa ananena khabari za kulala usiugizi. 14Bassi hapo Yesu akawaambia kwa wazi, Lazaro amekufa. 15Nami nafurahi kwa ajili yenn kwamba sikuwa huko, mpate kuamini: lakini na twende kwake. 16Bassi Tomaso, aitwae Didumo, akawaambia wanafunzi wenziwe, Twende na sisi, tufe pamoja nae.
17Bassi alipofika Yesu, akamkuta amekwisha kuwa kaburini yapata siku nne. 18Na Bethania ilikuwa karibu ya Yerusalemi, kadiri ya stadio khamstashara; 19na watu wengi katika Wayahudi wamekuja kwa Martha na Mariamu, illi kuwafariji kwa ajili ya ndugu yao. 20Bassi Martha, aliposikia kwamba Yesu anakuja, akaenda kumlaki; na Mariamu alikuwa akikaa nyumbani. 21Bassi Martha akamwambia Yesu, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu asingalikufa. 22Lakini hatta sasa najua ya kuwa vyovyote utakavyomwomba Mungu, Mungu atakupa. 23Yesu akamwambia, Ndugu yako atafufuka. 24Martha akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho. 25Yesu akamwambia, Mimi ni ufufuo na uzima; aniaminiye mimi, ijapo afe, atakuwa ataishi, 26na killa mwenye uzima na kuniamini mimi hatakufa kabisa hatta milele. Je! waamini haya? 27Akamwambia, Naam, Bwana; mimi nimeamini ya kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajae ulimwenguni. 28Na alipokwisha kusema haya, akaenda zake, akamwita dada yake, Mariamu, kwa siri, akisema, Mwalimu yupo, anakuita. 29Nae aliposikia, akaondoka upesi, akamwendea. 30Na Yesu alikuwa hajafika ndani ya kijiji, lakini alikuwa pale pale alipomlaki Martha. 31Bassi wale Wayahudi waliokuwa pamoja nae nyumbani, wakimfariji, walipomwona Mariamu, jinsi alivyoondoka upesi na kutoka, wakamfuata, wakidhani ya kuwa anakwenda kaburini illi alie huko. 32Bassi Mariamu, alipofika pale alipokuwapo Yesu, akamwona, akaanguka miguuni pake, akamwambia, Bwana, kama ungaliwapo hapa, ndugu yangu asingalikufa. 33Bassi, Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana nae wanalia, akaugua rohoni, akajifadhaisha nafsi yake, 34akasema, Mmemweka wapi? Wakamwambia, Bwana, njoo, utazame. 35Yesu akatoka machozi. 36Bassi Wayahudi wakanena, Angalieni jinsi alivyompenda. 37Bali wengine walisema, Je! huyu aliyemfumbua macho yule kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife?
38Bassi Yesu akiugua tena nafsini mwake akatika kaburini. Nalo lilikuwa pango, na jiwe limewekwa juu yake. 39Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule mtu aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa: maana amekuwa mayiti siku nne. 40Yesu akamwambia, Sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu? Bassi wakaliondoa lile jiwe. 41Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. 42Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia siku zote; lakini kwa ajili ya makutano hawa wanaozunguka nalisema haya, wapate kuamini kwamba ndiwe uliyenituma. 43Akiisha kusema haya, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, toka, njoo huku. 44Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa saanda miguuni na mikononi, na uso wake umefungwa kitambaa. Yesu akawaambia, Mfungueni, kamwacheni aende zake.
45Bassi wengi katika Wayahudi waliokuja kwa Mariamu na kuyaona aliyoyafanya Yesu, wakamwamini. 46Lakini baadhi yao wakaenda zao kwa Mafarisayo, wakawaambia aliyoyafanya Yesu. 47Bassi makuhani wakuu na Mafarisayo wakakusanya baraza, wakanena, Tunafanya nini? Maana mtu huyu afanya ishara nyingi. 48Tukimwacha hivi, watu wote watamwamini: na Warumi watakuja, wataondoa mahali petu na taifa letu. 49Mtu mmoja miongoni mwao, Kayafa, aliyekuwa kuhani mkuu mwaka ule, akawaambia, 50Ninyi hamjui neno lo lote, wala hamfikiri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu hawa, wala lisiangamie taifa zima. 51Na hili hakusema kwa nafsi yake, hali kwa kuwa alikuwa kuhani mkuu mwaka ule alitabiri ya kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa lile; 52wala si kwa ajili ya taifa lile tu, lakini pamoja na haya awakusanye watoto wa Mungu waliotawanyika wawe wamoja. 53Bassi tangu siku ile walifanya shauri wapate kumwua.
54Bassi Yesu hakutemhea tena kwa wazi kati ya Wayahudi, hali alitoka huko akaenda mahali karibu ya jangwa, hatta mji nitwao Efraim; akakaa huko pamoja na wanafunzi wake. 55Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; wengi wakapanda toka inchi yote pia kwenda Yerusalemi kabla ya Pasaka, illi wajitakase. 56Bassi wakamtafuta Yesu, wakasemezana wao kwa wao, wakisimama katika hekalu, Mwaonaje? Haji kabisa siku kuu hii? 57Na Makuhani na Mafarisayo wametoa amri ya kwamba, mtu akimjua alipo, alete khabari, wapate kumkamata.

Currently Selected:

Yohana MT. 11: SWZZB1921

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in