1
Mathayo 27:46
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Yapata saa tisa alasiri Yesu alilia kwa sauti kuu akisema, “ Eloi, Eloi, lema sabakthani? ” yaani “Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha peke yangu?”
Compara
Explorar Mathayo 27:46
2
Mathayo 27:51-52
Yesu alipokufa, pazia la Hekalu lilipasuka vipande viwili. Mpasuko wake ulianzia juu mpaka chini. Kulitokea pia tetemeko la ardhi na miamba ilipasuka. Makaburi yalifunguka na watu wengi wa Mungu waliokufa walifufuka kutoka kwa wafu.
Explorar Mathayo 27:51-52
3
Mathayo 27:50
Yesu akalia kwa sauti kuu tena, kisha akafa.
Explorar Mathayo 27:50
4
Mathayo 27:54
Afisa wa jeshi na askari waliokuwa wanamlinda Yesu walitetemeka sana kwa kuogopa tetemeko la ardhi na kila walichokiona kikitokea. Wakasema, “Hakika alikuwa Mwana wa Mungu!”
Explorar Mathayo 27:54
5
Mathayo 27:45
Ilipofika adhuhuri, giza liliifunika Israeli yote kwa muda wa masaa matatu.
Explorar Mathayo 27:45
6
Mathayo 27:22-23
Pilato akauliza, “Sasa nimfanye nini Yesu, aitwaye Masihi?” Watu wote wakasema, “Mwue msalabani!” Pilato akauliza, “Kwa nini mnataka nimwue Yesu? Amefanya kosa gani?” Lakini walipaza sauti wakisema, “Mwue msalabani!”
Explorar Mathayo 27:22-23
Inici
La Bíblia
Plans
Vídeos