Ndipo makuhani wakakutana na viongozi wazee wa Kiyahudi na kufanya mpango. Wakawalipa wale askari pesa nyingi na kuwaambia, “Waambieni watu kuwa wafuasi wake walikuja usiku na kuuiba mwili mlipokuwa mmesinzia. Gavana atakaposikia juu ya hili, tutazungumza naye ili msiadhibiwe.” Hivyo wale askari wakachukua pesa na kuwatii makuhani. Na jambo hili bado linasambaa miongoni mwa Wayahudi hata hivi leo.