Logo YouVersion
Eicon Chwilio

Mwanzo 2

2
1Kwa hiyo mbingu na dunia zikakamilika, pamoja na vyote vilivyomo.
2Kufikia siku ya saba Mungu alikuwa amekamilisha kazi aliyokuwa akiifanya; hivyo siku hiyo ya saba akapumzika kutoka kazi zake zote. 3Mungu akaibariki siku ya saba, akaifanya takatifu, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika baada ya kazi zote za kuumba alizokuwa amefanya.
Adamu na Hawa
4Haya ndio maelezo ya mbingu na dunia wakati zilipoumbwa.
Bwana Mwenyezi Mungu alipoziumba mbingu na dunia, 5hapakuwa na mche wa shambani uliokuwa umejitokeza ardhini, wala hapakuwa na mmea wa shamba uliokuwa umeota, kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mungu alikuwa hajanyeshea mvua juu ya nchi, na hapakuwa na mtu wa kuilima ardhi, 6lakini umande ulitokeza kutoka ardhini na kunyesha uso wote wa nchi. 7Bwana Mwenyezi Mungu alimuumba mtu kutoka mavumbi#2:7 Neno la Kiebrania la mavumbi ya ardhi ndilo kiini cha jina Adamu. ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, naye mtu akawa kiumbe hai.
8Basi Bwana Mwenyezi Mungu alikuwa ameotesha bustani upande wa mashariki, katika Edeni; huko akamweka huyo mtu aliyemuumba. 9Bwana Mwenyezi Mungu akafanya aina zote za miti ziote kutoka ardhini, miti yenye kupendeza macho na mizuri kwa chakula. Mti wa uzima ulikuwa katikati ya bustani, na pia mti wa kujua mema na mabaya.
10Mto wa kunyeshea bustani ulitiririka toka Edeni; kuanzia hapo ukagawanyika kuwa mito minne. 11Mto wa kwanza uliitwa Pishoni, nao huzunguka nchi yote ya Havila ambako kuna dhahabu. 12(Dhahabu ya nchi hiyo ni nzuri; bedola na vito shohamu pia hupatikana huko.) 13Jina la mto wa pili ni Gihoni, ambao huzunguka nchi yote ya Kushi. 14Jina la mto wa tatu ni Tigrisi, unaopita mashariki mwa Ashuru. Mto wa nne ni Frati.
15Bwana Mwenyezi Mungu akamchukua huyo mtu, akamweka kwenye Bustani ya Edeni ailime na kuitunza. 16Bwana Mwenyezi Mungu akamwagiza huyo mtu, akamwambia, “Uko huru kula matunda ya mti wowote katika bustani; 17lakini kamwe usile matunda ya mti wa kujua mema na mabaya, kwa maana siku utakapokula matunda yake, hakika utakufa.”
18Bwana Mwenyezi Mungu akasema, “Si vyema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa.”
19Basi Bwana Mwenyezi Mungu alikuwa ametengeneza kutoka ardhi wanyama pori wote, na ndege wote wa angani. Akawaleta kwa huyu mtu aone atawaitaje, nalo jina lolote alilokiita kila kiumbe hai, likawa jina lake. 20Hivyo Adamu akawapa majina mifugo wote, ndege wa angani, na wanyama pori wote.
Lakini kwa Adamu hakupatikana msaidizi wa kumfaa. 21Hivyo Bwana Mwenyezi Mungu akamfanya Adamu kulala usingizi mzito, naye alipokuwa amelala akachukua moja ya mbavu zake, akapafunika mahali pale kwa nyama. 22Kisha Bwana Mwenyezi Mungu akamfanya mwanamke kutoka kwa ule ubavu alioutoa kwa mwanaume, akamleta huyo mwanamke kwa mwanaume.
23Huyo mwanaume akasema,
“Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu,
na nyama ya nyama yangu,
ataitwa ‘mwanamke’,
kwa kuwa alitolewa katika mwanaume.”
24Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
25Adamu na mkewe wote walikuwa uchi, wala hawakuona aibu.

Dewis Presennol:

Mwanzo 2: ONMM

Uwcholeuo

Rhanna

Copi

None

Eisiau i'th uchafbwyntiau gael eu cadw ar draws dy holl ddyfeisiau? Cofrestra neu mewngofnoda