1
Luka 17:19
Neno: Maandiko Matakatifu
Isa akamwambia, “Inuka na uende zako, imani yako imekuponya.”
Vergleichen
Studiere Luka 17:19
2
Luka 17:4
Kama akikukosea mara saba kwa siku moja na mara saba kwa siku moja akaja kwako akisema, ‘Ninatubu,’ msamehe.”
Studiere Luka 17:4
3
Luka 17:15-16
Mmoja wao alipoona kwamba amepona, akarudi kwa Isa, akimsifu Mungu kwa sauti kuu. Akajitupa miguuni mwa Isa akamshukuru. Yeye alikuwa Msamaria.
Studiere Luka 17:15-16
4
Luka 17:3
Kwa hiyo, jilindeni. “Kama ndugu yako akikukosea mwonye, naye akitubu, msamehe.
Studiere Luka 17:3
5
Luka 17:17
Isa akauliza, “Je, hawakutakaswa wote kumi? Wako wapi wale wengine tisa?
Studiere Luka 17:17
6
Luka 17:6
Bwana Isa akawajibu, “Kama mkiwa na imani ndogo kama punje ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu, ‘Ng’oka ukaote baharini,’ nao ungewatii.
Studiere Luka 17:6
7
Luka 17:33
Mtu yeyote anayejaribu kuyaokoa maisha yake atayapoteza, na yeyote atakayeyapoteza maisha yake atayaokoa.
Studiere Luka 17:33
8
Luka 17:1-2
Isa akawaambia wanafunzi wake, “Mambo yanayosababisha watu watende dhambi hayana budi kutukia. Lakini ole wake mtu yule anayeyasababisha. Ingekuwa heri kama mtu huyo angefungiwa jiwe la kusagia shingoni na kutoswa baharini, kuliko kumsababisha mmojawapo wa hawa wadogo kutenda dhambi.
Studiere Luka 17:1-2
9
Luka 17:26-27
“Kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku za Mwana wa Adamu. Watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka siku ile Nuhu alipoingia katika safina. Ndipo gharika ikaja na kuwaangamiza wote.
Studiere Luka 17:26-27
Home
Bibel
Lesepläne
Videos