1
Luka 3:21-22
Swahili Revised Union Version
Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu zilifunuka; Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua; sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe.
مقایسه
Luka 3:21-22 را جستجو کنید
2
Luka 3:16
Yohana alijibu akawaambia wote, Kweli mimi nawabatiza kwa maji; lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuilegeza kamba ya viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto
Luka 3:16 را جستجو کنید
3
Luka 3:8
Basi, toeni matunda yapatanayo na toba; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Abrahamu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Abrahamu watoto.
Luka 3:8 را جستجو کنید
4
Luka 3:9
Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa kwenye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.
Luka 3:9 را جستجو کنید
5
Luka 3:4-6
kama ilivyoandikwa katika kitabu cha maneno ya nabii Isaya; Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake. Kila bonde litajazwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipopindika patakuwa pamenyoka, Na palipoparuza patalainishwa; Na wote wenye mwili watauona wokovu wa Mungu.
Luka 3:4-6 را جستجو کنید
خانه
كتابمقدس
برنامههای مطالعه
ویدیوها