Yohana 16
16
1 #
Yn 14:29
Maneno hayo nimewaambia, msije mkakwazwa. 2#Yn 9:22; Mt 5:11; 24:9; Lk 6:22 Watawatenga na masinagogi; naam, saa inakuja kila mtu awauaye atakapodhania ya kuwa anamfanyia Mungu ibada. 3#Yn 15:21 Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi. 4#Lk 22:53; Yn 17:12 Lakini nimewaambia hayo, ili makusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi niliwaambia.
Kazi ya Roho
Sikuwaambia hayo tangu mwanzo, kwa sababu nilikuwapo pamoja nanyi. 5#Yn 7:33 Lakini sasa mimi naenda zangu kwake yeye aliyenituma, wala hakuna mmoja wenu aniulizaye, Unakwenda wapi? 6Ila kwa sababu nimewaambia hayo huzuni imejaa mioyoni mwenu. 7#Yn 14:16,26 Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitamtuma kwenu. 8#1 Kor 14:24; Ebr 4:12 Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu. 9#Yn 3:18; Rum 1:18 Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi; 10#Mdo 5:31; Rum 4:25 kwa habari ya haki, kwa sababu mimi naenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena; 11#Yn 12:31; 14:30 kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa. 12#1 Kor 3:1 Hata bado ningali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamuwezi kuyastahimili hivi sasa. 13#Yn 14:26; 1 Yoh 2:27 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. 14Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari. 15#Yn 17:10 Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nilisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari.
Huzuni itageuka kuwa furaha
16 #
Yn 14:19
Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni; na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona.
17Basi baadhi ya wanafunzi wake wakasemezana, Neno gani hilo asemalo, Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona? Na hilo, Kwa sababu naenda zangu kwa Baba? 18Basi walisema, Neno gani hilo asemalo; hilo, Bado kitambo kidogo? Hatujui asemalo. 19Yesu alifahamu ya kwamba wanataka kumwuliza, akawaambia, Ndilo hilo mnaloulizana, ya kuwa nilisema, Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona? 20Amin, amin, nawaambia, Ninyi mtalia na kuomboleza, bali ulimwengu utafurahi; ninyi mtahuzunishwa, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha. 21#Isa 26:17 Mwanamke azaapo, ana huzuni kwa kuwa saa yake imefika; lakini akiisha kuzaa mwana, haikumbuki tena ile dhiki, kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtu ulimwenguni. 22#Isa 66:14 Basi ninyi hivi sasa mna huzuni; lakini mimi nitawaona tena; na mioyo yenu itafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleaye. 23#Yn 14:13,14,20; 1 Yoh 5:14; Mt 7:7; Mk 11:24 Tena siku ile hamtaniuliza neno lolote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lolote atawapa kwa jina langu. 24#Yn 15:11 Hata sasa hamjaomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.
Amani kwa wanafunzi
25 #
Yn 10:6
Hayo nimesema nanyi kwa mithali; saa inakuja ambapo sitasema nanyi tena kwa mithali, lakini nitawapa waziwazi habari ya Baba. 26Na siku ile mtaomba kwa jina langu, wala siwaambii ya kwamba mimi nitawaombea kwa Baba; 27#Yn 14:21 kwa maana Baba mwenyewe awapenda kwa kuwa ninyi mmenipenda mimi, na kusadiki ya kwamba mimi nilitoka kwa Baba. 28Nilitoka kwa Baba, nami nimekuja hapa ulimwenguni; tena nauacha ulimwengu; na kwenda kwa Baba. 29#Yn 16:25 Basi wanafunzi wake wakasema, Tazama, sasa wasema waziwazi, wala huneni mithali yoyote. 30#Yn 2:25 Sasa tumejua ya kuwa wewe wafahamu mambo yote, wala huna haja ya mtu akuulize; kwa hiyo twasadiki ya kwamba ulitoka kwa Mungu. 31Yesu akawajibu, Je! Mnasadiki sasa? 32#Zek 13:7; Mt 26:31,45; Mk 14:27,50; Yn 8:29 Tazama, saa inakuja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke yangu; lakini mimi siko peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami. 33#Yn 14:27; Rum 5:1; 1 Yoh 5:4 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.
اکنون انتخاب شده:
Yohana 16: RSUVDC
هایلایت
به اشتراک گذاشتن
کپی
می خواهید نکات برجسته خود را در همه دستگاه های خود ذخیره کنید؟ برای ورودثبت نام کنید یا اگر ثبت نام کرده اید وارد شوید
The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013.