1 Mose 9
9
Maongozi mapya.
1Mungu akambariki Noa na wanawe na kuwaambia: Zaeni wana, mwe wengi, mwijaze nchi!#1 Mose 1:28. 2Nyama wote wa nchi nao ndege wote wa angani sharti wawaogope ninyi na kuwastuka, wote pia wanaotembea katika nchi nao samaki wote wa baharini wametiwa mikononi mwenu. 3Nyama wote wanaotembea wenye uzima ni chakula chenu; kama nilivyowapa maboga yenye majani, ninawapa sasa wao wote nao.#1 Mose 1:29; Kol. 2:16. 4Lakini nyama walio wazima bado, maana walio wenye damu zao msiwale!#3 Mose 3:17. 5Nazo damu zenu na roho zenu nitazilipiza, kweli nitazilipiza kwa nyama wote nako kwa watu, roho ya mtu nitailipiza kwa mtu mwenziwe.#2 Mose 21:28-29; 1 Mose 4:11; 2 Mose 21:12. 6Atakayemwaga damu ya mtu damu yake nayo sharti imwagwe na mtu, kwa kuwa Mungu alimfanya mtu kwa mfano wake.#3 Mose 24:17; Mat. 26:52; Ufu. 13:10. 7Nanyi zaeni wana, mwe wengi! Ijazeni nchi mkiwa wengi huku!#1 Mose 1:27.
Maagano ya Mungu.
8Kisha Mungu akamwambia Noa na wanawe waliokuwa naye kwamba: 9Tazameni, mimi sasa ninawawekea agano langu ninyi nao wa uzao wenu wajao nyuma yenu#1 Mose 6:18. 10nao nyama wote wenye uzima waliokuwa nanyi: ndege na nyama wa nyumbani na nyama wote wa porini waliokuwa nanyi, wao wote waliotoka mle chomboni, ndio nyama wote pia wa huku nchini.#Hos. 2:18. 11Nalo agano langu, ninalowawekea ninyi, ni hili: Wao wote wenye miili hawatatoweshwa tena na mafuriko ya maji, wala hayatakuwako tena mafuriko ya maji ya kuiangamiza nchi.#1 Mose 8:21-22.
Upindi wa Mungu.
12Kisha Mungu akasema: Agano hili, mimi ninalolifanya nanyi nao nyama wote wenye uzima wanaokaa kwenu, litakuwa nalo lao vizazi vya kale na kale, nacho kielekezo chake ni hiki: 13nimeuweka upindi wangu mawinguni, nao utakuwa kielekezo cha agano, mimi nililoliagana na nchi. 14Itakapokuwa, nikitanda mawingu mengi juu ya nchi, huo upindi utaoneka mawinguni; 15ndipo, nitakapolikumbuka agano langu mimi, nililoliagana nanyi nao wote wenye roho za uzima, ndio wote wenye miili, ya kwamba: Hayatakuwako tena mafuriko ya maji ya kuwaangamiza wote wenye miili. 16Upindi huo utakapokuwa mawinguni, nitautazama, nilikumbuke agano la kale na kale, mimi Mungu nililoliagana nao wote wenye roho za uzima, ndio wenye miili wote wanaokaa huku nchini. 17Kisha Mungu akamwambia Noa: Hiki ndicho kielekezo chaagano, nililokuwekea wewe nao wenye miili wote wanaokaa huku nchini.
Kiapizo na mbaraka ya Noa.
18Wana wa Noa waliotoka chomboni walikuwa Semu na Hamu na Yafeti, naye Hamu ndiye baba yao Wakanaani. 19Hawa watatu walikuwa wana wa Noa; toka kwao hawa watu wakaineza nchi yote. 20Noa alipoanza kulima shamba, akapanda shamba la mizabibu. 21Lakini alipokunywa mvinyo akalewa, akalala hemani pasipo kujifunika. 22Hamu, baba yao Wakanaani, alipouona uchi wa baba yake, akawasimulia ndugu zake wawili huko nje.#Fano. 30:17. 23Ndipo, Semu na Yafeti walipochukua nguo, wakaiweka mabegani kwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao, macho yao yakitazama mbele, wasiuone uchi wa baba yao. 24Noa alipolevuka katika ulevi wa mvinyo, naye alipoyatambua, mwanawe mdogo aliyomfanyizia, 25ndipo aliposema:
Kanaani na awe ameapizwa!
Sharti awe mtumwa wa watumwa kwa ndugu zake!
26Kisha akasema:
na atukuzwe Bwana, Mungu wa Semu!
Naye Kanaani sharti awe mtumwa wake!#Rom. 9:16.
27Mungu na ampanulie naye Yafeti,
apate kukaa mahemani mwa Semu!
Naye Kanaani sharti awe mtumwa wake!#Ef. 3:6.
28Baada ya mafuriko ya maji Noa akawapo miaka 350. 29Hivyo siku zote za kuwapo kwake Noa zikawa miaka 950, kisha akafa.
Currently Selected:
1 Mose 9: SRB37
Tya elembo
Share
Copy
Olingi kobomba makomi na yo wapi otye elembo na baapareyi na yo nyonso? Kota to mpe Komisa nkombo
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.